Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikito taarifa ya kifo
cha Nahodha wa timu ya 94 Green Warriors, Ikongo Julius Mbaga
aliyefariki dunia jana alfajiri (Februari 17, 2017) kwenye Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa.
Mchezaji
huyo alijeruhiwa kwenye ajali ya gari ya timu yake iliyotokea Februari
13, 2017 Ihumwa mkoani Dodoma wakati ikiwa njiani kwenda Shinyanga
kucheza mechi ya Ligi Daraja la Pili (SDL) dhidi ya Bulyanhulu FC.
Taratibu
za mazishi ya Marehemu ambaye mwili wake umehamishiwa Hospitali Kuu ya
Jeshi (GMH) ya Lugalo jijini Dar es Salaam zinafanywa na familia yake
kwa kushirikiana na klabu ya 94 Green Warriors. Taarifa rasmi za mazishi
zitatolewa baadaye.
TFF
imetuma salamu za rambirambi kwa familia ya Marehemu, klabu ya 94 Green
Warriors na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na
kuwataka kuwa na uvumilivu kwa kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Kwa
Msiba huu, Rais wa TFF Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa
Mwenyekiti wa 94 Green Warriors, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na
marafiki kwa msiba huo mkubwa wa mpendwa wao.
Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani katika makazi yake ya milele.
Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani katika makazi yake ya milele.
0 Maoni:
Post a Comment