Nahodha
wa Simba, Jonas Mkude amesema kwamba hawaihofii timu yoyote
watakayokutana nayo mbele yao na dhamira yao ni kukifunga kikosi
chochote watakachokutana nacho.
Kauli
hiyo ya Mkude imekuja baada ya Simba kufanya vizuri katika mechi zake
tatu ambapo mbili ni za Ligi Kuu Bara na moja ya hatua ya 16 Bora ya
Kombe la FA.
Simba
imezifunga Majimaji (3-0) na Prisons kwa idadi kama hiyo ya mabao
katika mechi za ligi kuu halafu ikaifunga African Lyon bao 1-0 katika
Kombe la FA.
Simba
ambao wapo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 51,
Februari 25, mwaka huu watacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mkude
amesema kuwa, wao wamejiwekea lengo la kushinda mechi zao tisa
zilizobakia bila ya kuangalia aina gani ya timu wanayokutana nayo.
“Muhimu
kwa sasa ni kushinda tu hakuna jambo lingine kwa ajili ya kutimiza kile
tulichokianza tangu mwanzoni mwa msimu huu ambacho ni kuhakikisha
tunatwaa ubingwa wa ligi kuu.
“Haitajalisha
nani tunacheza naye bali kikubwa ni kushinda pekee na hilo tunataka
kulitimiza kwenye mechi hizi tisa zilizobakia kama ambavyo tumekuwa
tukishinda katika mechi nyingine,” alisema Mkude.
0 Maoni:
Post a Comment