Yanga
haijafanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake na tayari imeanza
mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa mabao 5-1,
hivyo Mkurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm amesema
watafika mbali.
Pluijm
ambaye ni raia wa Uholanzi ameliambia Championi Jumamosi kuwa, Yanga
itafika mbali kwenye michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf)
kutokana na mwenendo mzuri ambao wameanza nao msimu huu.
Leo
Jumamosi Yanga inatarajiwa kurudiana na Ngaya Club de Mbe ya Comoro
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya awali kushinda mabao 5-1
huko Moroni, Comoro.
Pluijm
ambaye amewahi kuifundisha timu ya Berekum Chelsea ya Ghana, alisema
ana uhakika wa Yanga kufanya vizuri kwani ina kikosi kilichokaa pamoja
kwa muda mrefu, hivyo wana nafasi nzuri ya kupata ushindi.
“Ni
mwanzo mzuri ambao tumeanza nao na ushindi huo tulioupata utakuwa chachu
kwetu ya kuendelea kupata matokeo mazuri kwenye michuano hiyo.
“Kama
tukiendelea kufanya hivi katika kila mechi, basi tuna kila sababu ya
kufika mbali kutokana na kikosi kipana tulichonacho, pia wachezaji hawa
wamekaa pamoja muda mrefu.
“Wachezaji
wengi wana uzoefu na michuano hii na hilo ndilo linalonipa zaidi
msukumo wa kusema Yanga itafika mbali na utaamini maneno yangu baadaye,”
alisema Pluijm.
Msimu
uliopita, Yanga iliishia raundi ya tatu katika Ligi ya Mabingwa Afrika
kisha ikatua katika Kombe la Shirikisho ambako iliishia hatua ya
makundi.
0 Maoni:
Post a Comment