SIMBA
hii Leo wana nafasi murua ya kutwaa uongozi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom,
ikiwa wataifunga Tanzania Prisons kwenye Mechi itakayochezwa Uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam.
Ushindi
kwa Simba, chini ya Kocha kutoka Cameroon Joseph Omog, utawafanya wawe
na Pointi 51 na kuwatoa Yanga, walio na Pointi 49, uongozini.
Wikiendi
hii Yanga hawachezi VPL kwa vile Jumapili wako huko Comoro kucheza na
Ngaya kwenye Mechi yao ya Kwanza ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ
LIGI.
Simba
watatinga kwenye Mechi hii wakiwa na ari kubwa kwani, baada ya kuyumba
kwa kipigo, waliibuka Wikiendi iliyopita kwa kuitwanga Majimaji 3-0 huko
Songea.
Leo
pia zipo Mechi nyingine 3 za VPL ambazo Stand United watakuwa wenyeji
wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga wakati
Ndanda FC ikiialika Toto Africans kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona,
Mtwara na Ruvu Shooting ikicheza na Azam FC kwenye Uwanja wa Mabatini,
Pwani.
Jumapili,
Mwadui FC itacheza Mbeya City kwenye Uwanja wa Mwadui wakati African
Lyon itacheza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na pia JKT
Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
0 Maoni:
Post a Comment