Kikosi
cha Azam FC leo Jumamosi inacheza na Stand United kwenye uwanja wake wa
Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam na habari njema kwa
mashabiki wa timu hiyo ni kwamba John Bocco amereja.
Kocha
Msaidizi wa Azam, Idd Nassor ‘Cheche’ ameliambia Championi Jumamosi
kuwa, wanautumia mchezo huo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand kama sehemu
ya maandalizi yao ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya
Mbabane Swallows ya Swaziland wikiendi ijayo.
Cheche
alisema kikosi chake kipo vizuri kuelekea mchezo huo wa kimataifa ikiwa
ni pamoja na kufanya vyema kwenye ligi ili kuweza kumaliza katika
nafasi nzuri ya msimamo wa ligi.
“Tumejiandaa
vizuri na mechi yetu dhidi ya Stand United, tunahitaji kushinda mchezo
huo ambao tunautumia kujiandaa na mechi yetu ya kimataifa dhidi ya
Mbabane Swallows.
“Wachezaji
wetu wote wapo vizuri na John Bocco amerejea rasmi kwani tulimchezesha
dakika chache katika mechi iliyopita ili kuweza kuona kiwango chake, ila
sasa yupo fiti kabisa,” alisema Cheche.
“Wachezaji wote wanaonyesha morali ya hali ya juu katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zote zilizobakia za ligi.”
0 Maoni:
Post a Comment