Kiungo mshambuliaji mwenye makeke wa
Mbeya City, Mrisho Ngassa, amejiapiza kuwa kamwe hawatakubali kufanywa
daraja la kuipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara Klabu ya Simba.
Mbeya City na Simba, zinakutana leo
Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mechi ya ligi kuu huku
Simba ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo uliopita.
Katika mechi iliyopita kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, mabao ya Simba yalifungwa na Mohamed Ibrahim ‘Mo’ na Ibrahim Ajibu.
Ngassa alisema kwa maandalizi waliyoyafanya chini ya Kocha Kinnah Phiri, anaamini yanatosha kuwapa ushindi kwenye mchezo huo.
Ngassa alisema, hawataki kupoteza mchezo
dhidi ya Simba kwa lengo la kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo baada
ya kupoteza 'Mbeya Derby' na Tanzania Prisons waliovaana nao katika
Kombe la FA ambao walitolewa kwa mikwaju ya penalti.
“Sitaki kutoa ahadi ya mabao
tutakayoshinda na badala yake mimi binafsi nitaipambania timu yangu
kuhakikisha tunaibuka na ushindi ili tumalize ligi kuu tukiwa katika
nafasi nzuri.
"Simba ni timu ya kawaida kama
zilivyokuwa timu nyingine na kwa bahati nzuri timu hiyo niliwahi
kuichezea, hivyo ninawafahamu nusu ya wachezaji niliokuwa nacheza nao
pamoja,” alisema Ngassa.
0 Maoni:
Post a Comment