Simba
leo Jumamosi inacheza na Mbeya City mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, klabu hiyo imesema wapinzani wao
wamekuja wakati mbaya kwao.
Kocha
wa Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon, amesema Mbeya City imekuja
kipindi ambacho timu yake inataka ushindi kwa lazima ili wawe katika
nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.
Omog
alisema pia Mbeya City inakutana na beki Juuko Murshid ambaye hakuwepo
kikosini tangu kuanza kwa mwaka huu. Juuko, raia wa Uganda, Januari,
mwaka huu, alikuwa Gabon akiiwakilisha nchi yake katika Kombe la Mataifa
ya Afrika.
Simba
ina pointi 54 kileleni mwa ligi hiyo ikifuatiwa na Yanga yenye pointi
52, wakati Mbeya City ikiwa nafasi ya nane na pointi 29 huku Mtibwa
Sugar ikiwa na pointi 33 katika nafasi ya tano.
“Wapinzani
wetu wamekuja wakati mbaya sana, kwani sisi tunasaka pointi tatu kwa
juhudi zote ili wasipotee katika mbio za ubingwa, pili ni kurejea kwa
beki wetu Juuko.
“Safu yetu ya ulinzi imeimarika kuweza kupambana na timu yoyote.”
Akizungumzia
mchezo huo, Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri, raia wa Malawi, alisema:
“Tumejipanga kushinda mchezo huu, kikosini tuna nyota wengi wenye
uzoefu, tutawatumia kuifunga Simba.”
0 Maoni:
Post a Comment