USIKU
huu huko Anfield Jijini Liverpool, Wenyeji Liverpool wanatinga kucheza
na Arsenal kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, inayokutanisha Timu
ambazo zipo Nafasi za 4 na 5.
Arsenal wako Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 50 kwa Mechi 25 na Liverpool ni wa 5 wakiwa wamecheza Mechi 26 na wana Pointi 49.
Mechi
hii ni ngumu hasa ukiangalia Takwimu zake kwani Liverpool wameshinda
Mechi 1 tu wakiwa kwao Anfield katika 9 zilizopita na hiyo ilikuwa 5-1
Februari 2014 na nyingine kwenda Sare 5 na Kufungwa 3.
Lakini
mapema Msimu huu, kwenye EPL huko Emirates Jijini London, Liverpool
iliinyuka Arsenal 4-3 hapo Agosti 14 kwa Bao za Coutinho, Bao 2, Lallana
na Sadio Mane huku Arsenal wakifunga kupitia Theo Walcott,
Oxlade-Chamberlain na Chambers.
Mbali ya ugumu wa Mechi yenyewe, pia hata Mameneja wa Timu hizi mbili nao wako kwenye presha kubwa.
Jurgen
Klopp sasa ameanza kupondwa waziwazi na Mashabiki wa Liverpool hasa
baada ya Jumatatu iliyopita kuchabangwa Bao 3-1 na Mabingwa Watetezi
Leicester City huko King Power Stadium na kuonyesha kupoteza mwelekeo
kwenye EPL.
Nae
Arsene Wenger, hasa baada ya kudundwa 5-1 na Bayern Munich kwenye UEFA
CHAMPIONZ LIGI huko Munich, huku pia akipoteza mwelekeo kwenye EPL hasa
kipindi hiki kama kawaida yao, amekuwa akisakamwa ang’oke.
**************************************
JE UNAIJUA HII?
- Arsène Wenger ataingia kwenye Gemu yake ya 50 dhidi ya Liverpool na Leo anapigana asifungwe na Liverpool kwa mara ya Pili katika Msimu mmoja wa EPL kitu ambacho mara ya mwisho kilitokea Mwaka 2000.
**************************************
Kwenye Gemu kama hii ya EPL iliyochezwa Anfield Msimu uliopita, Timu hizi zilitoka Sare ya 3-3.
Majeruhi
- Liverpool: Ings, Ejaria, Sturridge na Henderson [Huenda akacheza].
- Arsenal: Elneny na Cazorla
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
LIVERPOOL: Mignolet, Clyne, Matip, Lovren, Milner, Lallana, Can, Wijnaldum, Mane, Firmino, Coutinho
Akiba watatokana na:
Karius, Manninger, Origi, Klavan, Moreno, Stewart, Henderson, Randall,
Alexander-Arnold, Woodburn, Ojo, Wilson, Gomez, Henderson, Lucas
ARSENAL: Cech, Bellerin, Mustafi, Koscielny, Monreal, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Xhaka, Welbeck, Sanchez, Ozil
Akiba watatokana na: Ospina,
Martínez, Jenkinson, Debuchy, Mertesacker, Gabriel, Holding, Gibbs,
Ramsey, Maitland-Niles, Iwobi, Reine-Adélaïde, Sanogo, Walcott, Pérez,
Giroud.
REFA WA MCHEZO HUO: Robert Madley
0 Maoni:
Post a Comment