MANCHESTER
UNITED Leo inatinga Uwanja wao wa Nyumbani Old Trafford kucheza Mechi
yao ya EPL, Ligi Kuu England, na Bournemouth wakiwa na uwezo wa kupanda
hadi Nafasi ya 4 wakishinda lakini Meneja wao Jose Mourinho ametangaza
lengo lao sasa ni kumaliza Nafasi ya Pili Msimu huu.
Man
United hawajafungwa katika Mechi 16 za EPL na sasa wapo Nafasi ya 6
wakiwa Pointi 15 nyuma ya Vinara Chelsea kitu ambacho Mourinho ameona
kuutamani Ubingwa Msimu huu ni kitu kisichowezekana lakini kwa Nafasi ya
Pili inawezekana kwa vile Tottenham, walio Nafasi ya Pili, wapo Pointi 5
mbele yao.
Jana
Mourinho ameeleza: “Nafasi ya Pili ni ngumu lakini inawezekana. Ya
Kwanza haiwezekana ila ya Pili inawezekana na inabidi tuipiganie!”
Aliongeza: “Halafu tupiganie EUROPA LIGI nayo ni ngumu lakini tupo kwenye Tiumu 16 za mwisho! Kwa sasa tunacheza na Bournemouth, tunacheza na Chelsea [FA CUP Robo Fainali] na tunacheza na Rostov [EUROPA LIGI], na kisha tutaona tuko wapi.”
Kuhusu
Mechi ya Leo, Man United itamkosa Henrik Mkhitaryan ambae anasumbuliwa
na Misuli ya Pajani wakati Bournemouth Majeruhi wao ni Francis, Wilson
na Federici.
Bournemouth wako katika hali tete na hawajashinda Mechi yeyote ya Mashindano yote katika Mechi 8 zilizopita.
Mara ya mwisho wao kushinda ni Tarehe 31 Desemba 2016.
Mara
ya mwisho kwa Bournemouth kuivaa Man United ni Mwaka Jana Agosti 14
kwenye Mechi ya ufunguzi ya Msimu mpya wa EPL huko Vitality Stadium na
Man United kushinda 3-1 kwa Bao za Juan Mata, Wayne Rooney na Zlatan
Ibrahimovic huku Adam Smith akiipa Bournemouth Bao lao.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
MAN UNITED: De Gea, Valencia, Smalling, Bailly, Blind, Carrick, Herrera, Mata, Pogba, Rashford, Ibrahimovic
Akiba kutokana na:
Subs from Pereira, Fosu-Mensah, Tuanzebe, Young, Schweinsteiger,
Lingard, Rojo, Romero, Rooney, Shaw, Darmian, Martial, Fellaini
BOURNEMOUTH: Boruc, Cook, Mings, Daniels, Arter, Surman, Stanislas, Wilshere, Fraser, King
Akiba kutokana na: Allsop, Jordan, B Smith, Cargill, Mousset, Gosling, Ibe, Pugh, Ramsdale, Gradel
REFA: Kevin Friend
0 Maoni:
Post a Comment