ARSENAL
wanatarajiwa kutoa Ofa ya Pauni Milioni 60 ili kumnunua Straika wa Lyon
ya France Alexandre Lacazette baada ya kukata tamaa ya kuweza kumbakiza
Alexis Sanchez kwa ajili ya Msimu ujao.
Mpaka
sasa Fowadi wao kutoka Chile Sanchez bado hajakubali kusaini Mkataba
mpya huku wa sasa ukiwa umebakiza Miezi 18 tu na Meneja wa Arsenal
Arsene Wenger inadaiwa ashakata tamaa ya kuendelea kuwa nae.
Hilo limemfanya Wenger kutafuta mbadala wake na Lacazette yupo juu kabisa ya Listi ya walengwa wake.
Ripoti huko England na France zimedai Lyon itadai ilipwe si chini ya Pauni Milioni 50 na Dau halisi kufikia Pauni Milioni 60 ikitegemea vigezo zaidi vya mafanikio ya Mchezaji huyo.
Kabla Msimu huu wa sasa kuanza Arsenal walitoa Ofa ya Pauni Milioni 35 kumnunua Lacazette lakini ilikataliwa na Lyon na sasa Dau limepanda wakati pia Liverpool wakiripotiwa kumnyemelea.
Licha ya kuwafungia Lyon Bao 27 katika Mechi zao 31 Msimu huu Lyon wako tayari kumuuza Lacazette kwa Dau kubwa muafaka kwao.
0 Maoni:
Post a Comment