Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa sasa atakuwa anaonekana tofauti baada ya kupiga upara.
Chirwa amepiga upara siku chache kabla ya Yanga kwenda kuivaa Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa.
Yanga itashuka dimbani kesho Jumamosi kuivaa Azam FC katika mechi kali na Chirwa akitegemewa kuwa kiongozi wa ushambulizi.
Baada ya picha yake kuonekana mitandaoni, mashabiki wamekuwa wakijadili kwamba kwa nini Chirwa ameamua kunyoa?
Wengine wanaamini anataka kuwatisha Azam FC na wengine wanaamini huenda ni mtindo tu akitaka kuonekana tofauti.
0 Maoni:
Post a Comment