ALEXIS
Sanchez ameendelea kujikusanyia tuzo klabuni Arsenal hii ni baada ya
Alhamisi usiku kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi
Machi.
Sanchez
mwenye umri wa miaka 28 sasa ameibuka mshindi baada ya kupata asilimia
63.3 ya kura zote zilizopigwa na mashabiki wa klabu hiyo.
Ikumbukwe
Machi,Sanchez aliifungia Arsenal mabao mawili kwenye michezo ya kombe la
FA na ligi kuu dhidi ya vilabu vya Lincoln City na West Bromwich
Albion.
Pia alitoa pasi moja ya goli lililofungwa na Danny Welbeck kwenye
mchezo dhidi ya Liverpool ulioisha kwa Arsenal kulala kwa goli 3-1.
Nafasi ya
pili imetwaliwa na Theodore Walcott aliyepata kura asilimia 19.9 huku
Granit Xhaka akishika nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia asilimia 16.8
ya kura zote.
Hiyo inakuwa ni tuzo ya tano kutwaliwa na Sanchez msimu huu,mara nyingi zaidi klabuni Arsenal.
0 Maoni:
Post a Comment