![]() |
Phil Jones (pili kushoto) anaonekana kuumia baada ya kukabiliwa na Chris Smalling (kati) wakati wa mazoezi |
Mabeki wa Manchester United Chris
Smalling na Phil Jones walipata majeraha ya kuwaweka nje kwa muda mrefu
walipokuwa wanachezea timu ya taifa ya England, meneja wa klabu hiyo
Jose Mourinho amesema.
Jones, 25, aliumia kwenye kidole wakati wa mazoezi akikabana na mpinzani.
Taarifa zinasema kisa hicho kilimhusisha Smalling.
Beki mwenzake Smalling, 27, alipigwa picha akiwa amefungwa kitambaa mguuni baada ya kuumia pia wakati wa mazoezi.
Nahodha
wa United Wayne Rooney hata hivyo amepata nafuuu na atarejea kuwachezea
dhidi ya West Brom leo Jumamosi baada ya kupona jeraha la goti.
Rooney, 31, alikosa mechi United za karibuni zaidi walizocheza United.
Kutokana na kuumia kwa Smalling na Jones, Mourinho amemwita beki wa miaka 19 Axel Tuanzebe kikosini kwa ajili ya mechi hiyo.
Tuanzebe amechezea United mechi moja pekee ya ushindani, mechi ambayo waliilaza Wigan 4-0 katika Kombe la FA Januari.
United watakuwa pia bila mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na kiungo wa kati Ander Herrera wanaotumikia adhabu.
Pia, watamkosa Paul Pogba, anayeuguza jeraha la misuli ya paja.
0 Maoni:
Post a Comment