Eden Hazard anatarajiwa kubakia Chelsea na kusaini Mkataba Mpya wakati Nahodha wao John Terry akipewa nyongeza ya Mwaka Mmoja.
Vigogo
wa Spain Real Madrid wamehusishwa na kumnasa Hazard, mwenye Miaka 26,
kwa Dau la Pauni Milioni 100 pamoja na kuwapa Chelsea Mchezaji Mmoja
lakini Meneja Antonio Conte amekataa na kusisitiza Hazard atabaki
Chelsea huku pia Mmiliki wao Roman Abramovich akikataa kabisa kuuzwa kwa
Mbelgiji huyo.
Vilevile
habari hizi zimedai kuwa hata mwenyewe Hazard hataki kuondoka London
ambako Msimu huu amefunga Bao 14 kwa Chelsea na Belgium.
Ripoti hizo pia zimedai Mkataba Mpya wa Hazard hapo Chelsea utampa Mshahara wa £300,000 kwa Wiki.
Wakati
huo huo, imefahamika kuwa Nahodha wa Chelsea John Terry amepewa Mkataba
Mpya wa kubakia kwa Mwaka Mmoja zaidi ambao utamfanya awe Stamford
Bridge kwa Msimu wake wa 20.
Terry, mwenye Miaka 36, aliongezewa Miezi 12 Msimu uliopita baada ya kumalizika Mkataba wake.
Licha ya kuvumishwa Msimu huu ndio mwisho wa Terry, Meneja Conte amesisitiza kuwa Terry bado ni muhimu mno kwa Klabu.
0 Maoni:
Post a Comment