BAADA
ya Mechi za Kimataifa kwa Wiki Mbili, La Liga ya huko Spain ilianza
tena Jana kwa Mechi 1 na itaendelea Leo kwa Mechi 4 na Kesho Jumapili
kupigwa Mechi 4 ambazo pia zitashirikisha Vinara Real Madrid kuwa kwao
Santiago Bernabeu na Mabingwa Watetezi Barcelona kucheza Ugenini.
Hapo Jana, Espanyol, wakiwa kwao, waliichapa Real Betis 2-1.
Moja ya Mechi za hii Leo, ni ya Timu ya 4 Atletico Madrid kucheza Ugenini na Malaga.
Jumapili,
Real Madrid, ambao wanaongoza La Liga wakiwa Pointi 2 mbele ya Barca
huku pia wakiwa na Mechi 1 mkononi, wapo kwao Santiago Bernabeu kucheza
na Deportivo Alaves ambao wako Nafasi ya 10 na wako Pointi 25 nyuma ya
Real.
Kwenye Mechi yao ya kwanza ya La Liga Msimu huu, Real, wakicheza Ugenini, waliitwanga Alaves 4-1.
Nao
Barca wako Ugenini kucheza na Granada ambayo ipo Mkiani kwenye Nafasi ya
19 na ambayo pia waliifunga 1-0 katika Mechi ya Kwanza ya La Liga Msimu
huu iliyochezwa Nou Camp hapo Mwezi Oktoba.
LA LIGA:Ratiba:
@@Saa za Bongo
Jumamosi Aprili 1
1400 Villarreal CF v SD Eibar
1715 Osasuna v Athletic de Bilbao
1930 Real Sociedad v CD Leganes
2145 Malaga CF v Atletico de Madrid
Jumapili Aprili 2
1300 Sevilla FC v Sporting Gijon
1715 Real Madrid CF v Deportivo Alaves
1930 Valencia C.F v Deportivo La Coruna
2145 Granada CF v FC Barcelona
Jumatatu Aprili 3
2145 Celta de Vigo v Las Palmas
Jumanne Aprili 4
2030 Athletic Club v Espanyol
2230 Atlético Madrid v Real Sociedad
Real Betis v Villarreal
Jumatano Aprili 5
2030 Barcelona v Sevilla
2130 Deportivo La Coruna v Granada
2130 Sporting Gijón v Málaga
2130 Deportivo Alavés v Osasuna
2230 Leganés v Real Madrid
Alhamisi Aprili 6
2030 Eibar v Las Palmas
2230 Valencia v Celta de Vigo
0 Maoni:
Post a Comment