>>> >>>>>>>> NI KILIO KWA WADAU WA ‘NI ARSENAL FC SI ARSENE FC’!
Arsene
Wenger amedokeza kubakia Klabuni Arsenal pale alipotoboa anafanya
mipango kwa ajili ya Msimu Mpya lakini akasema Wachezaji Wapya watatua
hapo kwa ajili ya Klabu na si yeye.
Hata hivyo, Wenger amesisitiza mipango ya Msimu Mpya anaifanya hata kama angekuwa anaondoka mwishoni mwa Msimu huu.
Habari
hizi zitakuja kama pigo kubwa kwa Washabiki wanaoshinikiza Wenger
aondoke kwa kutoleta mafanikio yeyote tangu 2004 walipotwaa Ubingwa wa
England kwa mara ya mwisho.
Wadau hao, wenye Kampeni iliyobatizwa ‘NI ARSENAL FC SI ARSENE FC’,
ni wazi watakatishwa tamaa na habari hizi baada ya presha yao kupamba
moto hasa baada ya Arsenal kucharazwa 10-2 katika Mechi 2 na Bayern
Munich na kutupwa nje ya UCL, UEFA CHAMPIONZ kwenye Raundi ya Mtoano ya
Timu 16 ikiwa ni mara ya 7 mfululizo kufeli Hatua hiyo ya Mashindano
hayo.
Inaelekea
sasa Wenger atasaini Mkataba Mpya wa Miaka Miwili na moja ya Wachezaji
Wapya ambao Wenger amependekeza watue Emirates ni Mchezaji wa Borussia
Dortmund, Marco Reus.
Pia
inasemekana Wenger sasa anasaka mbadala wa Mesut Ozil na Alexis Sanchez
ambao inadaiwa wako mbioni kuhama licha ya Wenger mwenyewe kutamka Juzi
wanataka kubaki na mazungumzo nao yanaendelea vizuri.
Akiosha
mikono kuwa Wachezaji wapya hutua Arsenal si kwa sababu yake, Wenger
ametamka: “Arsenal ni Brandi ya Dunia hivi Leo, inaheshimika Dunia
nzima. Jina la Arsenal ni kubwa kupita Jina langu na kuja Arsenal ni
muhimu…huji kwa Arsene Wenger..unakuja kwa Arsenal!”
0 Maoni:
Post a Comment