Gianni Infantino |
Shirikisho la soka duniani FIFA
chini ya raisi wake mpya Gianni Infantino linaonekana kujaribu kuinua
sana soka katika ukanda wa Afrika, ambako kuna wafuasi wengi wa
Infantino.
Shirikisho hilo la soka sasa limeamua kuipa Africa
nafasi ya upendeleo kwa kuiongezea nafasi 5 zaidi za ushiriki katika
fainali za kombe la dunia la mwaka 2026.
Katika fainali hizo timu
zitaongezeka kutoka 36 hadi 48 na Afrika itawakilishwa na timu 9 ambapo
nyingine ya 10 itapambana katika hatua ya mtoano.
Shirikisho hilo
pia limeongeza idadi ya timu kutoka katika bara la Ulaya ambapo mwanzoni
zilikuwa ni timu 13 na sasa zitakuwa 16, huku Marekani Kaskazini na
kusini zikiwa timu 6 badala ya 3.
Oceania nao wamepewa nafasi moja
ya uwakilishi wa moja kwa moja ambapo hapo mwanzo iliwapasa wacheze
mchezo wa mtoano na timu za Amerika Kusini ili kufudhu.
Hii
itawafanya New Zealand kuwa na nafasi kubwa ya kushiriki kombe la dunia
kila mara kutokana na kutokuwa na upinzani mkubwa haswa baada ya Australia
kuanza kushiriki michuano ya bara la Asia.
0 Maoni:
Post a Comment