Manchester United na Ajax Amsterdam zimetinga Fainali ya UEFA EUROPA LIGI baada kupeta Mechi zao za Marudiano za Nusu Fainali.
Man
United walitoka Sare 1-1 na Celta Vigo na wao kusonga kwa Jumla ya Bao
2-1 kwa vile walishinda 1-0 Wiki iliyopita huko Spain wakati Ajax
wamefungwa 3-1 lakini wamesonga kwa Jumla ya Bao 5-4 baada ya kushinda
Mechi ya Kwanza 4-1.
Man United walitangulia kufunga Dakika ya 17 kwa Bao la Kichwa la Marouane Fellaini alipounganisha Krosi ya Marcus Rashford.
Celta Vigo walisawazisha Dakika ya 86 kwa Bao la Kichwa la Fancundo Roncaglia.
Dakika
chache baada ya Bao hilo la kusawazisha, Refa aliwatoa kwa Kadi
Nyekundu Eric Bailly wa Man United na Roncaglia kwa kuvaana.
0 Maoni:
Post a Comment