Uhamisho wa Rekodi ya Dunia wa Dau la Pauni
Milioni 89.3 wa Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Manchester United
Mwezi Agosti Mwaka Jana unachunguzwa na FIFA.
Ingawa FIFA wamesisitiza kuwa huu si uchunguzi rasmi licha kutaka maelezo zaidi toka kwa Vilabu vilivyohusika.
Lakini
hatua hiyo imeshangaza kwani FIFA hao hao ndio wanaobariki Uhamisho wa
Wachezaji Kimataifa kupitia Mfumo wao wa International Transfer Matching
System (ITMS) ambao huhitaji taarifa zaidi ya 20 zikiwemo aina ya
Uhamisho, Mawakala wanaohusika, Ulipwaji wa Ada zote na namna
zitakavyolipwa.
Baada
ya hayo kutimizwa FIFA hutoa Kibali na hilo ndilo lililofanywa kwenye
Uhamisho wa Pogba na hivyo ndivyo ambavyo Klabu ya Manchester United
ilivyoijibu FIFA kwamba hawana cha ziada mbali ya yale yaliyokuwemo
kwenye ITMS.
Man
United ilipewa Cheti cha Uhamisho wa Kimataifa, ITC International
Transfer Certificate, mara baada ya kukamilisha taratibu zote za
Uhamisho wa Pogba kupitia Mfumo wa ITMS.
Lipi limejiri mpaka sasa FIFA kutaka Taarifa zaidi?
Mpaka sasa haijulikani kwanini FIFA wameibua haya kwa wakati huu.
Lakini Wachambuzi wanahisi kuwa hilo limetokana na kuchapishwa kwa Kitabu huko Germany Wiki hii, kiitwacho The Football Leaks: The Dirty Business of Football, ambacho,
miongoni mwa kulipua mengi nyuma ya pazia kuhusu Soka, pia kiligusia
ada kubwa mno aliyolipwa Wakala wa Pogba, Mino Raiola, kiasi cha kudaiwa
kuvunja Kanuni za FIFA za Uhamisho wa Wachezaji.
0 Maoni:
Post a Comment