Arsene Wenger amekiri kuwa Mpinzani wake wa Siku nyingi Sam Allardyce,
maarufu kama Big Sam, ni hatari kubwa katika azma ya Arsenal kufufua
matumaini yao kwenye mbio za Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England.
Sam
Allardyce hivi sasa ndio Meneja Mpya wa Crystal Palace ambayo Jumapili
Januari Mosi, 2017, Siku ya Kwanza ya Mwaka Mpya, itazuru Emirates
kucheza na Arsenal Mechi ya EPL.
Huko nyuma, wakati Allardyce akiwa Meneja wa Bolton Wanderers na West Ham, Wenger ashawahi kukwaruzana nae.
Hivi
sasa Arsenal wako Nafasi ya 4 kwenye EPL na Mechi hii na Palace ni
muhimu mno kwa Wenger na Arsenal yake kushinda ili wasitupwe mbali
kwenye mbio za Ubingwa.
Lakini,
kama ambavyo Wenger anavyotambua, Siku zote Timu za Big Sam hutumia
miguvu na Mipira ya moja kwa moja bila kulemba ili kuwayumbisha Arsenal
wanaopenda kumiliki mno Mpira.
Kwa
Allardyce hii itakuwa Mechi yake ya Pili kuiongoza Palace tangu
ateuliwe kuwa Meneja Wiki moja iliyopita na ya kwanza ilikuwa Droo ya
1-1 na Watford Siku ya Boksing Dei.
Nao Arsenal walishinda Mechi yao ya Boksing Dei 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion kwa Bao la mwishoni lakini kabla ya hapo walichapwa Mechi 2 mfululizo na Everton na Manchester City.
Wenger,
akiongea kuelekea Mechi hii na Palace, ameonyesha waziwazi kuihofia
Mechi hii kwa kusema:
“Ni muhimu mno kwa kila Timu kupigana kuwa juu.
Baada ya kupata Meneja Mpya ni wazi Palace watajiamini zaidi na kuwa na
mori zaidi. Hilo litafanya Gemu iwe ngumu mno. Chini ya Allardyce,
Palace ni hatari mno!”
Arsenal wako Pointi 9 nyuma ya Vinara Chelsea na ushindi dhidi ya Palace ni kitu cha kufa na kupona kwao.
HALI ZA WACHEZAJI
Arsenal
huenda wakamkosa Theo Walcott ambae ana maumivu ya Misuli ya Miguu
akiungana na Majeruhi Kieran Gibbs mwenye tatizo la Goti lakini
Sentahafu Shkodran Mustafi ameshapona tatizo la Misuli ya Pajani.
Pia
Wenger ameshatoboa kuwa Fowadi wao Danny Welbeck amepona tatizo la Goti
lililomuweka nje kwa muda mrefu na amerejea Mazoezini lakini kilichobaki
ni kuamua ni wakati gani muafaka kuanza kumtumia tena.
Kwa upande wa Palace, wao watamkosa Beki wao Damien Delaney ambae yuko Kifungoni.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
ARSENAL: Cech, Bellerin, Mustafi, Koscielny, Monreal, Coquelin, Xhaka, Sanchez, Ozil, Iwobi, Giroud
Akiba: Ospina, Martínez, Jenkinson, Gabriel, Holding, Elneny, Ramsey, Reine-Adélaïde, Sanogo, Pérez
CRYSTAL PALACE: Hennessey, MacArthur, Dann, Kelly, Ward, Flamini, Puncheon, Zaha, Cabaye, Townsend, Benteke
Akiba: Speroni, Fryers, Phillips, Wynter, Sako, Lee, Husin, McArthur, Ledley, Mutch, Campbell, Tomkins, Rémy
Andre Marriner ndio refa atakayechezesha mechi hii kati ya Arsenal vs Crystal Palace.
0 Maoni:
Post a Comment