LIVERPOOL Jana imemaliza Mwaka 2016 kwa ushindi mtamu kwao Anfield walipoitungua
Manchester City 1-0 na kubaki Nafasi ya Pili kwenye EPL, Ligi Kuu
England, wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea.
Kipigo
hiki kimewaacha City Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Liverpool
lakini wapo hatarini Leo kushushwa na Arsenal na Tottenham
wakishinda Mechi zao.
Bao
pekee na la ushindi kwenye Mechi hiyo lilifungwa Dakika ya 8 tu kwa
Krosi ya Adam Lallana iliyounganishwa kwa Kichwa safi cha Georginio
Wijnaldum.
LEO Januari Mosi zipo Mechi 2 za EPL kwa Watford kucheza na Tottenham na kisha Arsenal na Crystal Palace.
VIKOSI:
Liverpool: Mignolet, Clyne, Lovren, Klavan, Milner, Can, Henderson [Origi, 64’], Wijnaldum, Mane [Lucas, 89’], Lallana, Firmino.
Akiba: Karius, Sturridge, Moreno, Lucas, Origi, Ejaria, Alexander-Arnold.
Man City: Bravo,
Zabaleta [Jesus Navas, 86’], Otamendi, Stones, Kolarov, Fernandinho,
Toure [Iheanacho, 89’], Sterling, Silva, De Bruyne, Aguero.
Akiba: Sagna, Fernando, Caballero, Jesus Navas, Clichy, Iheanacho, Garcia.
0 Maoni:
Post a Comment