www.kiungomshambuliaji.blogspot.com inakuletea hii; Kocha wa Chelsea,
Antonio Conte anayejiita "the man himself" ambaye ameweka rekodi ya kipekee kwa
kuwa kocha wa kwanza kuwa ndani ya Epl kwa msimu wa kwanza kushinda
mechi 12 lakini pia kuvunja rekòdi ya Chelsea ya kushinda mechi 11
ameongelea kuhusu pesa zinazotolewa na Wachina.
Conte ambaye hivi
karibuni amemruhusu Oscar kwenda nchini China katika klabu ya Shanghai
SIPG inayofundishwa na Villa Boaz amesema
"Wachina
wanatoa pesa nyingi sana ukiangalia usajili wao wa Tevez ni
pesa nyingi
lakini pia kumtaka Ronaldo kwa pauni milioni 300 ni pesa
nyingi zaidi
Kulipwa mchezaji"
Conte alisisitiza kuwa "China wanapaswa
kuheshimu pesa, si kutoa pesa tu bali kutoa kwa mpangilio mzuri. Ni
ngumu mchezaji kukataa pesa wanazotoa China kwa kuwa ni nyingi sana"
Hivyo Conte hakubaliani na Pesa za Wachina anaona kama zinaharibu na
hazijengi. Ikumbukwe sasa Wachina wameanza kumsaka mwamuzi Mark
Clattenburg refa bora Duniani.
Mark Clattenburg |
Na ni malengo yao kuitangaza ligi yao lakini pia kukuza soka lao ili waweze kubeba kombe la Dunia miaka ijayo.
0 Maoni:
Post a Comment