Azam
FC ipo nafasi ya tatu na ina tofauti ya pointi 12 na vinara Simba
katika Ligi Kuu Bara, sasa imejigamba leo ni lazima iwafunge Majimaji
ugenini ili kupunguza utofauti wa pointi hizo.
Azam
ina pointi 26 katika mechi 16 ilizocheza ambapo kati ya hizo, imeshinda
mechi saba, imefungwa mara nne na imetoka sare mara tano, imefunga
mabao 21 na imefungwa mabao 14.
Mchezo
wa Azam na Majimaji unachezwa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea
mkoani Ruvuma na Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd amesema: “Lazima
tushinde.”
Timu
hizo zinakutana katika Uwanja wa Majimaji leo ambapo Azam ina historia
ya kutofungwa katika uwanja huo na wapinzani wao hao.
Akizungumza, Idd
alisema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na ametamba
wataendeleza ushindi wao kwa wapinzani wao hao ili wachukue pointi tatu
muhimu.
“Kocha
ameyafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza katika mechi yetu na
African Lyon na tuna imani tutafanya vizuri katika mchezo wetu wa kesho
(leo) ili kuweza kuendeleza rekodi yetu kwani hatujafungwa na Majimaji
katika uwanja wao.
“Kikosi
kipo vizuri na wachezaji wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo
isipokuwa tutawakosa wachezaji watatu ambao ni Daniel Amoah, Mudathir
Yahaya na Gadiel Michael ambao ni majeruhi,” alisema Idd.
Kwa
upande wake Kocha wa Majimaji, Kali Ongalla, alisema: “Mechi hii ni
ngumu, wenzetu wana wachezaji wengi wa kigeni, ila tutapambana ili
tushinde.”
0 Maoni:
Post a Comment