Hatimaye
Simba, Yanga na Azam FC zimemalizana na Idara ya Uhamiaji kwa kuwalipia
vibali vya kufanya kazi nchini wachezaji na watendaji wake wengine
klabuni.
Siyo
klabu hizo tu, hata African Lyon nayo jana kabla ya saa 7:00 mchana
ilikuwa imekamilisha taratibu zote za uhamiaji kwa wachezaji wake wa
kigeni.
Awali
Idara ya Uhamiaji ilizipiga mkwara klabu za Ligi Kuu Bara kutowatumia
wachezaji na watendaji wake wengine ambao ambao hawajatimiza taratibu za
uhamiaji ikiwemo kupewa kibali cha kufanya kazi nchini.
Uhamiaji
ilitoa muda hadi kufikia jana saa 7:00 mchana klabu hizo ziwe
zimekamilisha utaratibu wa kuwasilisha vibali vya makazi na vya kazi kwa
watendaji hao jambo lililotekelezwa na timu hizo.
Akizungumza
Ofisa wa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule alisema klabu
zote za mkoa wake ikiwemo African Lyon zimekamilisha taratibu zote hivyo
zinawaruhusiwa kuwatumia wachezaji na makocha wao.
“Nilitoa
muda hadi leo (jana) saa 7:00 mchana klabu zote ziwe zimekamilisha
taratibu zote za vibali kwa makocha na wachezaji wao na iwapo
wasingekamilisha basi wasingeruhusiwa kufanya kazi.
“Klabu
zote zimekamilisha zoezi hilo ikiwemo African Lyon, nimesimamia zoezi
hili kwa upande wa mkoa wangu hivyo iwapo kuna wachezaji wa mikoa
mingine ambao hawana vibali sijui,” alisema Msumule.
Kwa
mujibu wa Msumule, kibali cha ukaazi ni dola 2,050 kwa mwaka sawa na Sh
milioni nne na kile cha kufanyia kazi dola 1,000 kwa mwaka sawa na Sh
milioni mbili.
Waliolipiwa
kwa upande wa Simba ni wachezaji Javier Bokungu, Goue (Fredrick)
Blagnon, Laudit Mavugo, Daniel Agyei, James Kotei na Method Mwanjale
huku makocha wakiwa ni Kocha Mkuu Joseph Omog, Kocha Msaidizi Jackson
Mayanja na Kocha wa Makipa Idd Salim.
Kwa
upande wa Yanga, waliolipiwa ni Kocha Mkuu George Lwandamina,
Mkurugenzi wa Ufundi, Hans van Der Pluijm, Kocha wa Viungo, Noel
Mwandila na wachezaji ni Donald Ngoma, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe,
Vincent Bossou, Justine Zulu, Thabani Kamusoko na Obrey Chirwa.
Aidha,
baadhi ya wachezaji ambao vibali vyao vilikuwa bado ni pamoja na Donald
Ngoma, Laudit Mavugo, Amissi Tambwe, James Kotei na kwa upande wa
makocha wote wa timu hizo za Simba, Yanga na Azam.
Kwa
mujibu wa Msumule, Yanga ilikuwa imelipa baadhi ya vibali vya makazi
bila ya vya kazi lakini Simba haikuwa imelipa kibali chochote kwa
watendaji wake.
0 Maoni:
Post a Comment