KRC GENK YA UBELGIJI YAMTAKA THOMAS ULIMWENGU

Tokeo la picha la picha za thomas ulimwengu
Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ndiyo timu iliyotangaza rasmi kutaka kumnasa mshambuliaji Thomas Ulimwengu.

Ulimwengu ambaye ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na TP Mazembe, ameanza mazunguko na Genk ambayo anaichezea Mbwana Samatta.

Habari za uhakika, zimeeleza kuwa, Ulimwengu amekubali kujiunga na Genk licha ya ofa zaidi ya 10 kuwa mezani, lakini analazimika kusubiri.

“Analazimika kusubiri kidogo hadi wakati wa dirisha dogo wakati Genk watakapomuuza yule beki wao wa kati (Ndidi) raia wa Nigeria, anakwenda Leicester City kwa dau la pauni milioni 15,” kilieleza chanzo kutoka nchini Ubelgiji.
 Tokeo la picha la picha za thomas ulimwengu

Pamoja na Genk, taarifa zilieleza kuwa kuna timu nyingine mbili za Ubelgiji zimeonyesha kumtaka Ulimwengu lakini bado ni suala la makubaliano tu.

Alipoulizwa Meneja wa Ulimwengu, Jamal Kisongo kuhusiana na suala hilo, alisema: 
“Ulimwengu anatakiwa na zaidi ya timu kumi, kama mwanzo nilieleza tuko kwenye mazungumzo,” alisema Kisongo.

“Genk ni moja wapo, lakini kuna Oostende, pia kuna klabu kubwa kama Anderlecht. Lakini ni suala la kusubiri kwanza. Mambo yakiwa tayari, muwe na subira, tutawaeleza.” 


Ulimwengu ambaye alifanikiwa kubeba ubingwa wa Afrika akiwa na TP Mazembe, amekuwa na soko kubwa kutokana na mambo mawili. Moja ni mafanikio yake uwanjani na timu hiyo ya DR Congo, lakini kuwa mchezaji huru, pia inaonekana kuzivutia timu nyingi za barani Afrika na zile za Ulaya.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment