KIUNGO
wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan JANA DECEMBER 22 amezoa Tuzo yake ya 6
mfululizo kama Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Nchi yake Armenia.
Hii
ni Tuzo yake ya 7 tangu avuke Umri wa Miaka 20 na kumfanya awemo kwenye
Rekodi za Mastaa wa Dunia waliozoa mara nyingi Tuzo za aina hiyo.
Anaeongoza
kwa Tuzo aina hii kwa Nchi yake ni Mchezaji mwenzake Mkhitaryan huko
Man United, Zlatan Ibrahimovic, ambae amechukua mara 11.
Wengine
wanaomkimbiza Ibrahimovic ni Wachezaji toka Finland, Sami Hyypia,
alietwaa mara 9 na Jari Litmanen, mara 8, na Kipa wa Czech Republic Petr
Cech mara 8.
Lakini
hao wote wamestaafu Timu za Taifa wakati Mkhitaryan bado anacheza
akikimbizwa kwa karibu na wale ambao bado wanadunda Timu zao za Taifa
kina Gareth Bale wa Wales na David Alaba wa Austria, wote wakiwa na Tuzo
6 kila mmoja.
Wengine waliowahi kutwaa Tuzo 6 enzi zao ni Andriy Shevchenko wa Ukraine na Aliaksandr Hleb wa Belarus.
Walotwaa
mara 5 ni Marek Hamsik (Slovenia), Robert Lewandowski (Poland), Goran
Pandev (Macedonia) na Mstaafu Kakha Kaladze (Georgia).
Kwenye
baadhi ya Nchi Tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka zina mifumo tofauti kama
vile Portugal ambako zipo za aina mbili za yule achezae Ligi ya ndani na
yule achezae nje ya Nchi.
Huko, kwa Wachezaji wa nje, Cristiano Ronaldo amezoa mara 8 katika Miaka 10 iliyopita.
Na
Argentina wana mfumo wa aina hiyo hiyo ingawa kabla haijabaguliwa
Lionel Messi alibeba Tuzo mara 2 na ilipotofautishwa kati ya Wachezaji
wa ndani na nje, Messi alipewa mara 8 kati ya 9 kwa wa nje tangu wakati
huo.
0 Maoni:
Post a Comment