Mechi
14 za Ligi Kuu ya Vodacom zinatarajiwa kufanyika wakati huu wa msimu wa
kufunga mwaka 2016 na mbili za zitafungua mwaka 2017 ambako Kituo cha
Televisheni cha Azam - Wadhamini wenza wa ligi hiyo, wamethibitishia
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupata burudani kwa michezo
yote kulingana na ratiba.
Katika
Ligi hiyo ambayo pia inabarikiwa na Benki ya Diamond Trust (DTB),
michezo 15 ya kipindi cha sikukuu za kufunga na kufungua mwaka
inatarajiwa kuanza saa 10.00 jioni isipokuwa ule wa Mbao FC na Mwadui
uliopangwa kuanza saa 8.00 mchana kama itakavyojieleza hapo chini kwenye
mtiririko wa ratiba.
Burudani
kwa Wote katika michezo hiyo kutoka Azam Tv, zinaanzia mchezo wa leo
Ijumaa wa Desemba 23, mwaka huu ulipewa jina la Na. 129
utakaozikutanisha timu za African Lyon na Young Africans kwenye Uwanja
wa Uhuru, Dar es Salaam, Kamishna wa mchezo anatarajiwa kuwa Idelfonce
Magali kutoka Morogoro.
Katika
mchezo huo unaotarajiwa kuchezeshwa na Mwamuzi, Ludovic Charles kutoka
mkoani Tabora akisaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya (Mshika Kibendera Na.
1) na Alnord Bugado wa Singida (Mshika Kibendera Na. 2), Mwamuzi wa
Akiba – Mezani anatarajiwa kuwa Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam.
Jumamosi
Desemba 24, 2016 kutakuwa na mechi sita ukianzia ule wa Mbeya City na
Toto Africans zitacheza kwenye Uwanja wa Sokoine jijiji Mbeya katika
mchezo Na. 130 utakaosimamiwa na Kamishna George Komba wa Dodoma wakati
Mwamzi wa kati atakuwa Shakaile ole Shangalai wa Pwani huku wasaidizi
wake wakiwa ni Khalfan Sika pia wa Pwani na Vecent Milabu wa Morogoro.
Mwamuzi wa akiba atakuwa Cherles Mwamlima.
Mchezo
Na. 131 utazikutanisha timu za Kagera Sugar na Stand United katika
Uwanja wa Kaitaba, uliko Kagera ambako utasimamiwa na Kamishna
Nassoroi Hamduni wa Kigoma huku Mwamuzi akiwa ni Jacob Adongo wa Mara
akisaidiwa na Joseph Masija na Robert Luhemeja kutoka Mwanza na Mezani
atakuwa Jonesia Rukyaa wa Kagera.
Ndanda
itaendelea kubaki nyumbani kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara
na baada ya kucheza na Simba juma lililopita na kupoteza mchezo huo,
safari hii inaikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo Na. 132
utakaosimamiwa na Kamishna Jimmy Lengwe wa Morogoro wakati Mwamuzi
atakuwa Andrew Shamba wa Pwani akisaidiwa na Haji Mwalukuta wa Tanga na
Jeremiah Simon wa Dar es Salaam. Mezani atakuwa Abubakar Mtulo.
Siku
hiyo pia kutakuwa na mchezo kati ya Simba na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam. Mchezo huo Na. 133 utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar
es Salaam ambako utasimamiwa na Tito Haule wa Morogoro na kuchezeshwa
na Mwamuzi Hans Mabena wa Tanga. Mabena atasaidiwa na Omari Kambangwa wa
Dar es Salaam na Khalfan Sika wa Pwani wakati Mbaraka Rashid wa Dar es
Salaam atakuwa Mwamuzi wa Akiba – mezani.
Baada
ya kulala Mbeya mbele ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine,
Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Azam FC ya Dar es Salaam ambayo
juma lililopita iliambulia sare tasa kutoka kwa African Lyon. Majimaji
na Azam zinakutana kwenye mchezo Na. 134 utakaofanyika Uwanja wa
Majimaji mjini Songea.
Katika
mchezo huo ambao Mwamuzi atakuwa Ngole Mwangole wa Mbeya ambaye ni
mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita, atasaidiwa na
Mirambo Tshikungu na Mashaka Mwandembwa – pia wote wa Mbeya huku
kamishna akiwa ni David Lugenge wa Iringa.
Mwadui
ambayo ilianza vibaya duru la pili kwa kupoteza mchezo uliopita,
Jumamosi Desemba 24, mwaka huu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza
kwenye Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga. Mchezo huo Na. 135,
utasimamiwa na Kamishna Staricko Nyikwa wa Singida katika mchezo
utakaoanza saa 8.00 mchana ili kutoa fursa kwa mdhamini Azam kuonesha
mchezo huo moja kwa moja ikiwa na maana ya mubashara.
Waamuzi
wataongozwa na Emmanuel Mwandembwa atakayesimama katikati kupuliza
filimbi huku akisaidiwa na Abdallah Uhako na Agnes Pantaleo wote wa
Arusha na mezani anatarajiwa kuwa Ezekiel Mboi wa Shinyanga.
Krismas,
yaani Desemba 25, 2016 hakutakuwa na mchezo ila siku inayofuata Desemba
26, mwaka huu Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya
Mbeya kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani katika
mchezo Na 136.
Manyama
Bwire wa Dar es Salaam atakuwa Kamishna wa mchezo huo wakati Mwamuzi ni
Forentina Zabron wa Dodoma akisaidiwa na Hassan Zani wa Arusha na
Silvester Mwanga wa Kilimanjaro. Mwamuzi wa akiba - Mezani atakuwa
Andrew Shamba wa Pwani.
Desemba
28, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili ambako Young Africans ya Dar es
Salaam itakuwa mwenyeji wa Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru
jijini katika mchezo Na. 137 ambako Juma Chiponda wa Tanga atakuwa
kamishna wa mchezo huo.
Mwamuzi
wa kati katika mchezo huo atakuwa Eric Onoca wa Arusha akisaidiwa na
Michael Mkongwa wa Njombe na Janeth Balama wa Iringa. Mwamuzi wa akiba
atakayekaa mezani atakuwa Mwanahamisi Matiku wa Dar es Salaam.
Kadhalika
siku hiyo, Majimaji ya Songea itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro
kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Mvomero katika mchezo Na. 138
utakaosimamiwa na Kamishna Pius Mashera wa Dodoma, utachezeshwa na
Mathew Akrama kutoka Mwanza akisaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na
Gasper Ketto wa Arusha. Mwamuzi wa akiba atakuwa Selemani Kinugani.
Kadhalika
Desemba 29, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili. Ruvu Shooting ya Pwani
inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa
Uhuru Dar es Salaam katika mchezo ambao mwamuzi atakuwa Alex Mahagi wa
Mwanza.
Katika
mchezo huo Na. 139, Mahagi atasaidiwa na Ferdinand Chacha pia wa Mwanza
na Rashid Zongo wa Iringa huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hellen Mduma
wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Peter Temu wa Arusha.
Azam
ya Dar es Salaam itatulia nyumbani Uwanja wa Azam huko Chamazi ikicheza
na Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo Na. 140 utakaosimamiwa na
Elizabeth Kalinga wa Mbeya huku Mwamuzi akiwa ni Jimmy Fanuel wa
Shinyanga huku wasaidizi wake wakiwa ni Makame Mdog pia wa Shinyanga na
Abdallah Mkomwa wa Pwani huku Kassim Mpinga akiwa ni mwamuzi wa akiba.
Saa
kadhaa kabla ya kuingia mwaka 2017, yaani Desemba 31, mwaka huu
kutakuwa na michezo miwili ambako Mwadui ya Shinyanga itacheza na Kagera
Sugar ya Kagera kwenye Uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga katika mchezo
Na. 141.
Kamishna
anatarajiwa kuwa Nassib Mabrouk wa Mwanza na Mwamuzi ni Isihaka Mwalile
na wasaidizi wake ni Hellen Mduma na Omary Kambangwa – wote kutoka Dar
es Salaam. Julius Kasitu wa Shinyanga anatarajiwa kuwa Mwamuzi wa Akiba.
Kadhalika
siku ya funga mwaka, Mbeya City inatarajiwa kucheza na Mbao FC kwenye
Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika Mchezo Na. 143 ambao msimamizi wa
mchezo atakuwa Joseph Mapunda wa Ruvuma.
Mwamuzi
katika mechi hiyo anatarajiwa kuwa Hussein Athuman wa Katavi wakati
wasaidizi wake watakuwa ni Lulu Mushi wa Dar es Salaam na Nicholaus
Makaranga wa Morogoro. Mwamuzi wa Akiba Mezani atakuwa Mashaka
Mwandembwa wa Mbeya.
Januari
mosi kutakuwa na michezo miwili tu ya kukaribisha Mwaka Mpya ambako
Toto African ya Mwanza itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo Na. 144 utakaosimamiwa na Jovin
Bagenda wa Kagera. Mwamuzi atakuwa Israel Nkongo sambamba na wasaidizi
wake Soud Lila na Frank Komba, wote wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa akiba
mezani atakuwa Mathew Akrama wa Mwanza.
Pia
African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu katika
mchezo Na. 142 utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Kamishna
atakuwa Hamisi Kitila wa Singida wakati Mwamuzi anatarajiwa kuwa
Selemani Kinugani wa Morogoro wakati wasaidizi wake ni Omary Juma wa
Dodoma na Agnes Pantaleo wa Arusha wakati mezani atakuwa Shafii Mohammed
wa Dar es Salaam.
Mara
baada ya michezo hiyo, Ligi Kuu ya Vodacom itasimama kwa wiki mbili
kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Januari
mosi, mwaka huu.
0 Maoni:
Post a Comment