KUELEKEA MCHEZO WA AZAM FC VS MAJIMAJI FC




KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, LEO Jumamosi saa 10.00 jioni inatarajia kushuka dimbani kuwania pointi tatu muhimu mbele ya wenyeji wao, Majimaji, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Majimaji, mjini Songea, Ruvuma.

Azam FC itaingia dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu kwenye mchezo uliopita dhidi ya African Lyon huku Majimaji yenyewe ikipigwa bao 1-0 ugenini walipokipiga na maafande wa Tanzania Prisons.
Msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unaonyesha kuwa Azam FC kwa sasa ina pointi 26 katika nafasi ya tatu kwenye ligi huku wapinzani wao hao wakiwa nafasi ya 14 baada ya kujizolea pointi 16.

Katika mazoezi ya mwisho jioni hii, benchi la ufundi la Azam FC limeonekana kufanyia kazi madhaifu yote yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita pamoja na kujiandaa kikamilifu namna ya kuukabili Uwanja wa Majimaji, ambao hauko katika hali nzuri,

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Kocha Mkuu wa timu hiyo, Zeben Hernandez, amesema kuwa kikosi chake kipo vizuri kuelekea mtanange huo huku akidai kuwa amekipanga vilivyo kukabiliana na aina ya uwanja watakaochezea.

“Changamoto kubwa itakayokuwa kwenye mchezo huo ni uwanja, lakini hiyo sio kitu ni suala la kubadilisha fikra za wachezaji ili waweze kukabiliana na hali hiyo na hatimaye kuondoka na pointi tatu,” alisema.
Hernandez aliongeza kuwa: “Wachezaji wanatakiwa kuwa vizuri sana kwenye mchezo wa kesho ili kuweza kufanya maamuzi mazuri, pia hali ya kupambana inahitajika, naamini hivyo vitu vitatusaidia kupata pointi tatu kesho.”

Azam FC inayodhaminiwa na kinywaji safi cha Azam Cola kinacholainisha koo na kuburudisha mwili pamoja na Benki ya NMB, itaingia kwenye mchezo huo bila ya wachezaji wake wanne ambao ni wagonjwa, ambao ni mabeki Daniel Amoah, Abdallah Kheri, Ismail Gambo na kiungo Mudathir Yahya.

Rekodi zilipokutana (Head to Head)
Azam FC kihistoria imekutana mara saba na Majimaji kwenye mechi za ligi, Azam FC ikishinda asilimia 98 ya mechi hizo yaani tano, Majimaji ikiwa haijawahi kuonja pointi tatu dhidi yao huku ikishuhudiwa mechi mbili zikienda sare.
Mara ya mwisho timu hizo kukutana ndani ya uwanja huo ilikuwa ni mwaka jana, ambapo Azam FC ilishinda mabao 2-1, yaliyofungwa na Ame Ally na Didier Kavumbagu huku ile ya pili iliyofanyika Azam Complex ikiisha kwa kicheko tena kwa matajiri hao baada ya kuilaza 2-0, yote yakiwekwa kimiani na kiungo Mudathir Yahya.
 Tokeo la picha la PICHA WACHEZAJI WA AZAM
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment