BARCELONA WAINGIA UWANJANI BILA MSN (MESSI, SUAREZ NA NEYMAR)


Tokeo la picha la messi neymar suarez

MABINGWA wa Spain FC Barcelona Leo watatinga Uwanjani kwao Nou Camp kucheza Mechi yao ya mwisho kwa Mwaka 2016 bila ya Nyota wao Watatu, maarufu kama MSN, ambao wamepewa Likizo ya Mapema.

Baada ya Mechi hizi za Leo Soka la Spain linakwenda mapumziko ya Krismas na Mwaka Mpya na kurejea baada ya Wiki ya Kwanza ya Januari.
Lakini Kocha wa Barca Luis Enrique ameamua Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, ambao ndio hao MSN, pamoja na Gerrard Pique hawahitajiki kwa Mechi yao ya Leo na kuwaruhusu kwenda tangu walipomaliza Mechi yao ya Wikiendi walipoinyuka Espanyol 4-1.
Leo Barca wanarudiana na Timu ya Daraja la chini Hercules CF katika Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya Copa del Rey ambalo ni Kombe la Mfalme wa Spain.
Katika Mechi ya kwanza Timu hizi zilitoka 1-1.
COPA DEL REY
 Tokeo la picha la messi neymar suarez
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment