CAF
LEO imefanya Droo ya Mashindano ya CHAMPIONZ LIGI kwa Mwaka 2017 na
Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga wamepangwa kucheza na Ngaya Club ya
Comoro katika Raundi ya Awali.
Ikiwa Yanga watavuka watatinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi kati ya ZANACO ya Zambia na APR ya Rwanda.
Endapo Yanga watavuka tena hatua hiyo watatua Hatua ya Makundi.
Mabingwa
wa Zanzibar, Zimamoto, kwenye Raundi ya Awali, wataanza na Ferroviário
Beira ya Msumbiji na Mshindi kutinga Raundi ya Kwanza kucheza na Mshindi
wa Mechi ya Barrack Young Controllers ya Liberia na Stade Malien ya Mali.
Safari
hii Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI, ambayo sasa Kiudhamini yatajulikana
kama TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI, yamepanuliwa toka Mawili ya Timu 8 na
kuwa Timu 16 ambayo yatakuwa na Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.
Haya ni Mashindano ya 53 ya kusaka Klabu Bingwa Afrika lakini ni ya 21 tangu Mfumo wa CAF CHAMPIONZ LIGI uanze.
Mshindi
wa Mashindano haya atafuzu kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa
Duniani yatakayochezwa Mwaka 2017 huko United Arab Emirates na pia
kucheza CAF SUPER CUP dhidi ya Mshindi wa CAF Kombe la Shirikisho.
Bingwa Mtetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini
Iko sawa mkuu
ReplyDelete