NYOTA SABA WANAOCHEZA ULAYA WAIGOMEA CAMEROON AFCON 2017

Tokeo la picha la joel matip

 WACHEZAJI 7 wa Cameroon wamesema hawana nia ya kuichezea Timu ya Taifa ya Cameroon kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Africa, AFCON 2017, zitakazoanza Januari 14 huko Gabon.
 
Wachezaji hao 7, ambao waliteuliwa kwenye Kikosi cha Awali cha Wachezaji 35 na Kocha Hugo Broos mapema Mwezi huu, sasa wapo hatarini kufungiwa kuzichezea Klabu zao wakati AFCON 2017 ikiendelea.

Saba hao wote ni Maprofeshenali huko Ulaya nao ni Joel Matip (Liverpool), Andre Onana (Ajax Amsterdam), Guy Roland Ndy Assembe (Nancy), Allan Nyom (West Bromwich Albion), Maxime Poundje (Girondins Bordeaux), Andre-Frank Zambo Anguissa (Olympique Marseille) na Ibrahim Amadou (Lille).

Akiongea hapo Jana, Kocha wa Cameroon Broos amelalamika kuwa Wachezaji hao wameweka maslahi yao binafsi mbele kuliko ya Taifa na Shirikisho la Soka la Cameroon, FECAFOOT, lina haki ya kuwaadhibu kwa mujibu wa Kanuni za FIFA.

Matip, ambae ni Mzaliwa wa Germany, amedai yeye hataki kuichezea Cameroon kutokana na uhusiano mbovu na Makocha waliopita na amesusa kuichezea Cameroon tangu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 kwisha huko Brazil.

Mara mbili Kocha Broos alijaribu kumshawishi Matip lakini Mchezaji huyo aligoma.
Nao Nyom, by Amadou, Ndy Assembe, Onana na Zambo Anguissa wamemwambia Kocha huyo kuwa hawataki kuondoka Klabuni kwao kwa kuhofia kupoteza namba zao.

Nae Poundje, ambae hajawahi kuitwa na Cameroon nah ii ni mara ya kwanza kwake, amesisitiza kuwa nia yake ni kuichezea France.

Cameroon inatarajiwa kutangaza Kikosi chao cha mwisho kwa ajili ya AFCON 2017 mapema Wiki ijayo.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment