Hakuna ubishi kwamba Alexis Sanchez ana kipaji cha hali ya juu. Kwa
sasa yuko kwenye kiwango bora sana ‘on fire’ tangu alipoachana na
Barcelona na kujiunga na Arsenal moto wake umekuwa ni wa hatari sana
ndani ya Premier League.
PEP GUARDIOLA NA ALEXIS SANCHEZ
Tangu amekuwa akichezeshwa kama mshambuliaji wa kati na Arsene
Wenger, amekuwa akiimarika kila kukicha na kocha wake wa zamani Pep
Guardiola amekubaliana na hilo.
Akizungumza kuhusu mchezaji huyo wakati Manchester City inajiandaa
kuikabili Arsenal, Pep amekubali kwamba anadhani hakumtumia Sanchez
ipasavyo.
“Alicheza vizuri alivyokuwa Barcelona lakini kwa kawaida unapocheza na Messi wachezaji wote huwa hawafikii kiwango chake.”
“Nadhani Arsenal wanamtumia kama striker wa mbele, anafanya vizuri.
Tukiwa Barccelona nadhani sikumsaidia vya kutosha kwasababu alicheza
pembeni. Anaweza kucheza huko lakini ni bora akacheza mbele karibu na
goli.”
Alexis anafurahia Arsenal lakini kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na
The Gunners kuhusu mkataba mpya na anataka kuongezewa kiasi cha mshahara
ili asaini kkataba mpya kitu ambacho mashabiki wengi wa Arsenal
wanasema anastahili.
0 Maoni:
Post a Comment