HII NDIO SABABU ILIYOMFANYA DAVID LUIZ KUREJEA CHELSEA FC.


Kiungo mshambuliaji inakuletea hii ###### Beki wa Chelsea David Luis amezungumzia kurejea kwake tena ndani ya Chelsea baada ya kuondoka kwenda Paris Saint Germain, huku akisisitiza kuizimia Chelsea na kufurahia kurudi kwenye klabu hiyo.
Luiz amesema mambo yanakwenda haraka sana kwenye soka, alifurahi kupata nafasi ya kurudi na bado anafikiria nini kilisababisha awali klabu hiyo kumwacha aondoke.


 luiz-cfc
                                                         DAVID LUIZ


Wakati anazungumza na Sky Sports alisema: “Najaribu kusaidiana na wachezaji wenzangu pamoja na klabu ndio maana nimerudi.”
“Naipenda klabu kwasababu nilipata fursa na niliona ni lazima nirudi hapa.”
“Maamuzi yanafanyika haraka sana kwenye soka. Chelsea walipokuja kwangu na kuniambia wanataka mimi nirudi nilifurahi kwasababu nilikuwa na wakati mzuri wakati nipo hapa ni miongoni mwa sehemu bora katika career yangu.”
Luiz anasema kuna nyakati anatamani kuwa nahodha wa Chelsea, na kutokana na John Terry kuelekea ukingoni kwa muda wake wa kucheza, Luiz anaamini siku moja atavaa kitambaa cha unahodha.

Beki huyo wa kibrazil amekuwa nguzo muhimu kwenye safu ya ulinzi chini ya Antonio Conte na amekuwa akihusika kwenye matukio mengi ndani ya uwanja, kusaidia kwenye matukio ya kujitolea nje ya uwanja na kujenga umoja na wachezaji wenzake.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment