Kiungo mshambuliaji inakuletea hii ++++++ Baada ya ushindi wa Simba 2-0 Ndanda, kuwa na taarifa zinazoenea
kwenye mitandao ya kijamii kwamba huenda Simba ikapolwa pointi kwa kosa
la kuwachezesha wachezaji wawili wa kigeni (Daniel Agyei na James Kotei
wote kutoka Ghana) ambao bado hawajakamilisha vibali vya kufanyia kazi
nchini.
“Niseme hizo taarifa ni za uzushi ambazo zimeletwa na wapinzani wetu
ambao waliamini kwamba tutapoteza mchezo wetu dhidi ya Ndanda na wao
wataendelea kuwa juu ya msimamo wa ligi kwa hiyo ushindi wetu
haujawapendeza ndio maana wameamua kuendesha vita ya maneno ya uongo na
uchochezi,” amenukuliwa makamu wa rais wa Simba SC Geoffrey Nyange
Kaburu wakati akizungumza kwenye kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM.
“Simba imekamilisha taratibu zote za usajili ambazo zipo ndani ya
kanuni zetu za VPL, baada ya kukidhi mahitaji yote wachezaji husika
walipewa leseni na TFF na ndio ambazo zilitumiwa siku ya mchezo kwa hiyo
vijana wetu walikuwa na vigezo vyote vya kucheza dhidi ya Ndanda
kulingana na kanuni zetu.”
“Wanachama na wapenzi wa Simba wapuuzie haya maneno, kwa sasa lengo
letu ni kwenye mchezo wetu unaofata dhidi ya JKT Ruvu siku ya Jumamosi
na kubwa ni kuendelea kuvuna pointi na hilo ndio kiu ya wengi kuona timu
inashinda kila mechi na hatimaye kutwaa ubingwa.”
0 Maoni:
Post a Comment