SIKU YA MWISHO YA USAJIRI WA DIRISHA DOGO KWA CLUB YA SIMBA.

KIUNGO MSHAMBULIAJI INAKULETEA HABARI KUHUSU SIKU YA MWISHO YA USAJIRI KWA CLUB YA SIMBA YA JIJINI DAR-ES-SALAAM. December 15 2016 dirisha dogo la usajili la Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 linafungwa rasmi na tayari baadhi ya timu zimeshafunga usajili wake na kutoa list ya wachezaji wanaoendelea nao na walioachana nao.



Simba SC ni moja kati ya timu zilizofanya usajili dirisha dogo na imetaja majina ya wachezaji walioongezwa na kupunguzwa, Simba imewasajili golikipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei kutokea Ghana, Pastory Athanas wa Stand United na Juma Luzio kwa mkopo akitokea Zesco United ya Zambia.
Hata hivyo Simba imewapandisha wachezaji wawili kutoka timu B Vicent Costa na Moses Kitandu, walioachwa ni golikipa muivory coast Vincent Agban na kiungo mkongo Musa Ndusha, huku Awadhi Juma na Malika Ndeule wakitolewa kwa mkopo Mwadui FC na Emmanue Semwanza akienda Majimaji FC.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment