MABINGWA WATETEZI Bayern Munich wanaenda kwenye likizo ya Krismasi na
Mwaka Mpya wakiwa kileleni mwa Bundesliga baada ya Jana kuibonda Timu
iliyopanda Daraja Msimu huu RB Leipzig Bao 3-0.
Sasa Bayern wako mbele ya Timu ya Pili Leipzig kwa Pointi 3.
Bao za Bayern hapo Jana zilifungwa na Thiago na Xabi Alonso na
kisha Leipzig wakapata pigo Dakika ya 30 pale Emil Fosberg alipopewa
Kadi Nyekundu kwa kumchezea Rafu mbaya Philipp Lahm.
Robert Lewandowski akapiga Bao la 3 kwa Penati iliyotolewa baada ya Kipa wa Leipzig Peter Gulasci kumchezea Faulo Douglas Costa.
Licha ya kufungwa, kikiwa ni kipigo chao cha pili Msimu huu wao wa kwanza kwenye Bundesliga, Leipzig wako Nafasi ya Pili.
Chini ya Kocha Ralph Hasenhuttl, Leipzig wameshinda Mechi zao 11 za
kwanza za Bundesliga kati ta 15 ikiwa pamoja na kuifunga Timu ngumu
Borussia Dortmund
0 Maoni:
Post a Comment