Arda
Turan alipiga Bao 3 wakati Barcelona wakiichapa Timu ya Daraja la 3
Hercules 7-0 na kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey
kwenye Mechi iliyochezwa Nou Camp Jana Usiku.
Licha
ya Barca kutoka 1-1 na Hercules katika Mechi ya Kwanza, Kocha Mkuu wa
Barca, Luis Enrique, mara baada ya Barca kuitwanga Espanyol 4-1 katika
Mechi ya La Liga Juzi Jumapili, aliamua kuwapa likizo ya mapema Mastaa
wake Lionel Messi, Luis Suarez, Neymar na Pique likizo kwa vile Soka la
Spain litasimama hadi baada ya Wiki ya Pili ya Januari kupisha Sikukuu
za Krismasi na Mwaka Mpya.
Bila
ya hao Nyota, Barca waliongoza 2-0 hadi Mapumziko kwa Bao za Digne,
Dakika ya 37, na Rakitic, ikiwa ni Penati ya Dakika ya 45.
Kipindi cha Pili, Barca waliongeza Bao nyingine kupitia Rafinha, Dakika ya 50, Turan, 55, 86 na 89, na Alcácer, 73
Wakati
Timu nyingine Spain zikihenya kufunga Mwaka kwa Mechi hizi za Copa del
Rey, Real Madrid wao walicheza mapema Mechi zao za Kombe hili na kufuzu
kwa vile walikwenda Japan ambako Juzi walitwaa Kombe la Ubingwa wa Kombe
la Dunia kwa Klabu.
"Real Madrid ilikamilisha Mechi zake na kusonga kwa kuitwanga Cultural Leobesa Jumla ya Mabao 13-2 kwa Mechi 2"
RATIBA YA LEO USIKU MUDA KWA MASAA YA TANZANIA
Alhamisi Desemba 22
22:00 Deportivo Alaves v Gimnastica
22:00 Celta de Vigo v UCAM Murcia
23:00 Athletic de Bilbao v Real Racing Santander
23:00 RCD Espanyol v Alcorcon
0 Maoni:
Post a Comment