Beki kisiki wa Yanga, Vincent Bossou amejumuishwa katika kikosi cha
awali cha timu ya Taifa ya Togo kitachoshiriki Fainali za Kombe la
Mataifa Afrika mwezi ujao nchini Gabon.
Kocha mkuu Claude Le Roy pia ameendelea kumuamini mshambuliaji
Emmanuel Adebayor licha ya kutokuwa na timu tangu aachane na Crystal
Palace mwishoni mwa msimu uliopita.
Bossou anakuwa mchezaji wa tatu anayecheza Ligi Kuu Vodacom Tanzania
Bara kujumuishwa katika kikosi cha awali cha AFCON baada ya beki wa
Simba, Juuko Murshid kuteuliwa katika kikosi cha Uganda na Bruce Kangwa
wa Azam kujumuishwa katika kikosi cha Zimbabwe.
KIKOSI KAMILI CHA AWALI;
Walinda Milango: Kossi Agassa (Huru ), Baba Tchagouni (FC Marmande, Ufaransa), Cédric Mensah (Le Mans, Ufaransa)
Walinzi: Serge Akakpo (Trabzonspor, Uturuki), Sadate
Ouro-Akoriko (Al Khaleej, Saudia Arabia), Djene Dakonam (Saint-Trond,
Ubelgiji), Gafar Mamah (Dacia, Moldavie), Maklibè Kouloun (Dyto, Togo),
Hakim Ouro-Sama (AS Togo Port), Vincent Bossou (Young
Africans,Tanzania), Joseph Douhadji (Rivers United, Nigeria)
Viungo: Alaixys Romao (Olympiacos, Ugiriki),
Matthieu Dossevi (Standard Liège, Ubelgiji), Floyd Ayité (Fulham,
Uingereza), Henritsè Eninful (Doxa, Ujerumani ), Lalawele Atakora
(Helsingborgs, Sweden), Prince Segbefia (Goztepe, Uturuki), Ihlas Bebou
(Fortuna Dusseldorf, Allemagne), Franco Atchou (Dyto, Togo), Victor
Nukafu (Entente II, Togo), Serge Gakpe (Genoa, Italia)
Washambuliaji: Emmanuel Adebayor (Huru), Fo Doh Laba (Berkane, Morocco), Razak Boukari (Chateauroux, Ufaransa)
0 Maoni:
Post a Comment