Mshambuliaji Romelu Lukaku anatarajia mkataba mpya na klabu yake ya Everton ambao atakuwa akilipwa pauni 100,000.
Kwa kiwango hicho cha malipo, maana yake
Lukaku raia wa Ubelgiji ataweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa
Everton kulipwa kiasi hicho kwa wiki.
Everton ambayo nyumbani kwake ni Goodison Park jijini Liverpool, haijawahi kutoa pauni 100,000 kwa mchezaji yoyote.
Lukaku alijiunga na Everton Juni, 2019
akitokea Chelsea na imeelezwa wakala wake Mino Raiola amekuwa katika
mazungumzo mazito na uongozi wa Everton.
Katika majira ya joto, nusura Lukaku
arejee Chelsea lakini suala hilo lilishindikana baada ya mwekezaji mpya
wa Everton, Farhad Moshiri kusisitiza anataka abaki.
0 Maoni:
Post a Comment