Swansea wapo mbioni kumteua Paul Clement kama Meneja wao mpya.
Clement,
Bosi wa zamani wa Derby County na sasa yupo Bayern Munich kama Kocha
Msaidizi, amekuwa mazungumzoni na Swansea kuwa Meneja wao wa 3 Msimu
huu.
Huenda
mazungumzo hayo yakakamilika kabla ya Jumanne ambapo Swansea, wakiwa
mkiani mwa EPL, Ligi Kuu England, watasafiri kwenda London kucheza na
Crystal Palace.
Clement
anatarajiwa kurithi nafasi ya Bob Bradley alietimuliwa mara baada ya
Swansea kuchapwa 4-1 na West Ham Siku ya Boksing Dei baada ya kudumu kwa
Siku 85 tu.
Clement,
mwenye Miaka 44, alikuwemo kwenye usaili uliomteua Bob Bradley na
kuvutia kiasi cha Swansea kumtaka yeye sasa achukue nafasi hiyo.
Meneja huyu mtarajiwa amewahi kufanya kazi kama Msaidizi wa Carlo Ancelotti huko
Chelsea, Paris St Germain, Real Madrid na sasa Bayern Munich.
Lakini
kazi pekee aliyoifanya kama Meneja, huko Derby County, ilitibuka Miezi 8
tu tangu ateuliwe alipotimuliwa Februari 2016 bila kutegemewa kwani
aliiweka Derby Nafasi ya 5 baada kuongoza Ligi ya Daraja la Championship
Miezi Miwili nyuma.
0 Maoni:
Post a Comment