Kila kukicha Wachina wanaendelea kuwachanganya wachezaji mbalimbali katika timu zao. Hii inathibitishwa kwa wachina kutoa fedha nyingi katika usajiri wao, maana beki wa kati wa Real Madrid, Pepe naye anafikiria kwenda China.
Hii ni siku chache baada ya Carlos Tevez kukamilisha usajili wa kwenda China na atakuwa akipokea euro million 30 kila msimu.
Taarifa zinaeleza, Pepe anafikiria kwenda China na kujiunga na moja ya timu zinazoshiriki Super League.
Wachina wanaonekana kuanza kuwachanganya wachezaji mbalimbali kupitia fedha zao.
Klabu
za China zimekuwa zikiwalenga wachezaji mbalimbali maarufu kutoka
barani Ulaya wakiwemo wale wazaliwa wa Amerika Kusini ambao wanacheza
barani Ulaya.
0 Maoni:
Post a Comment