DAVID MOYES AREJEA KWA MARA YA KWANZA OLD TRAFFORD TANGU ALIPOTIMULIWA

 Sunderland boss David Moyes

LEO katika Moja ya Mechi 8 za EPL, Ligi Kuu England,ni ile itakayochezwa huko Old Trafford kati ya Manchester United na Sunderland na mvuto mkubwa ni kurejea tena Uwanjani hapo kwa David Moyes kwa mara ya kwanza tangu atimuliwe Umeneja na Man United Aprili 2014.

Mwenyewe Moyes ameshakiri kuwa ni kitu kisichowezekana kuendeleza urithi wa Meneja Lejendari Sir Alex Ferguson.

Lakini Meneja wa sasa wa Man United, Jose Mourinho, ametoboa anafurahia changamoto hizo na hataruhusu presha zimshinde.

Akiongea kuelekea mechi hii ya Leo, Mourinho ameeleza: “Sioni kama ni mzigo. Nahisi Historia kubwa ya Klabu hii ni kitu kizuri na siwazii mabaya. Tatizo ukipewa masharti ya kufuata!”
 Tokeo la picha la image man u vs sunderland

Alipoulizwa kama Moyes ndie alikuwa na changamoto kubwa kwani ndie alierithi moja kwa moja toka kwa Ferguson, Mourinho alijibu: “Sitajali kuwa kwenye Klabu yenye matumaini makubwa lakini kuwa nao Ryan Giggs, Nemanja Vidic, Patrice Evra na Chicharito kwenye Timu. Hilo sijali hata kidogo!”

Tahmini
Man United wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa wameshinda Mechi 4 mfululizo katika Mashindano yote na kuzoa Pointi 9 kati ya 9 kwenye EPL.
Sunderland, walioanza Msimu vibaya, walijikongoja Mwezi Novemba wakishinda Mechi 2 kati ya 3 na Mwezi huu walishinda Mechi zao 2 za Nyumbani dhidi ya Leicester na Watford na kuleta matumaini mapya.
Wakati Man United wapo Nafasi ya 6, Pointi 3 nyuma ya Timu ya 5 Tottenham na 4 nyuma ya Arsenal ambao ni wa 4, Sunderland wapo Nafasi ya 18 wakiwemo kwenye zile 3 za Mkiani ambazo hushuka Daraja mwishoni mwa Msimu.
Msimu uliopita:
Man United waliichapa Sunderland 3-0 Uwanjani Old Trafford kwa Bao za Wayne Rooney, Memphis Depay na Juan Mata na kufungwa 2-1 huko Stadium of Light..

Hali za Wachezaji:
Man United:
Hatihati: Bailly, Mkhitaryan [Bado hawajawa fiti kwa Mechi]
Majeruhi: Luke Shaw, Wilson

Sunderland:
Majeruhi:Rodwell (hamstring, 14 Jan), Gooch (ankle, Mar), Cattermole (hip, Apr), Kirchoff (knee, Apr), McNair (knee, Aug), Watmore (knee, Aug)
**Adnan Januzaj haruhusiwi kuichezea Sunderland kwenye Mechi hii kutokana na Mkataba wake wa Mkopo kutoka Man United.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
MAN UNITED: De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian, Carrick, Herrera, Mkhitaryan, Pogba, Martial, Ibrahimovic
Akiba: Romero, Depay, Lingard, Fosu-Mensah, Tuanzebe, Schneiderlin, Young, Blind, Fellaini, Schweinsteiger, Bailly, Rashford, Rooney, Mata, Smalling

SUNDERLAND: Pickford, Jones, Kone, Djilobodji, Van Aanholt, Denayer, Ndong, Khazri, Borini, Anichebe, Defoe
Akiba: Mannone, Love, Manquillo, O’Shea, Larsson, Pienaar, Honeyman, Asoro, E Robson, J Robson, T Robson

REFAMartin Atkinson
 Tokeo la picha la image man u vs sunderland

**Saa za Bongo
Jumatatu Desemba 26
1530 Watford v Crystal Palace              
1800 Arsenal v West Bromwich Albion            
1800 Burnley v Middlesbrough              
1800 Chelsea v Bournemouth               
1800 Leicester City v Everton               
1800 Manchester United v Sunderland            
1800 Swansea City v West Ham United           
2015 Hull City v Manchester City 


Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment