LEO EPL, Ligi Kuu England, ipo Mechi 1 tu huko Anfield kati ya Liverpool na Stoke City.
Katika
Mechi ya mwisho hapo Jana, Man City iliitandika Hull City 3-0 kwa Bao
za Yaya Toure, Penati, Iheanacho na Davies aliejifunga mwenyewe.
Liverpool
wanashikilia Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 37 sawa na Timu ya 4 Arsenal
na kuzidiwa na Timu ya Pili Manchester City Pointi 2 huku Vinara wakiwa
Chelsea wenye Pointi 46. Stoke City wapo Nafasi ya 12 wakiwa na Pointi 21.
Liverpool
wataingia kwenye Mechi hii wakimkosa Majeruhi Philippe Coutinho lakini
Beki wao Joel Matip ameshapona na huenda akapewa nafasi.
Kwa
Stoke, Fowadi wao Marko Arnautovic bado yupo Kifungoni baada ya
kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi na Southampton mapema Mwezi huu.
Uso kwa Uso
Liverpool wameshinda Mechi 5 kati ya 6 zilizopita za EPL dhidi ya Stoke na Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii walishinda 4-1.
Katika
kipindi hicho, Mechi pekee Stoke waliyoshinda ni Bao 6-1 kwenye Mechi
ambayo ilikuwa ya mwisho kabisa kwa Nahodha wao maarufu Steven Gerrard.
Pia
Stoke walishinda 1-0 Mwezi Januari katika Mechi ya Pili ya Nusu Fainali
ya Kombe la Ligi ingawa walishindwa Nusu Fainali hiyo kwa Mikwaju ya
Penati Tano Tano zilizopigwa baada ya Mechi 2 za Nusu Fainali kufungana.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
LIVERPOOL: Mignolet, Clyne, Lovren, Klavan, Milner, Lallana, Henderson, Wijnaldum, Mane, Origi, Firmino
STOKE CITY: Grant, Johnson, Shawcross, Martins Indi, Pieters, Whelan, Imbula, Diouf, Allen, Krkic, Walters
REFA: Michael Oliver
MSIMAMO LIGI KUU UINGEREZA
0 Maoni:
Post a Comment