www.kiungomshambuliaji.blogspot.com inakuletea hiiLIGI za Ulaya, mara nyingi sikukuu ya Krismasi hutumika kama kigezo cha dalili za timu fulani kuwa bingwa.
Mfano,
timu zilizokuwa kileleni wakati wa Krismasi, asilimia kubwa
zilifanikiwa kubeba ubingwa mwishoni mwa msimu. Zipo ambazo ziliboronga
mwishoni zikafeli.
Ligi
kubwa za Ulaya zina timu 18 hadi 20. Utaona unapofikia msimu wa
Krismasi, nyingi ndiyo zinakuwa zimekaribia kumaliza mzunguko wa kwanza
ambao unatakiwa kuwa na mechi 19 au 17.
Kwa
Tanzania kidogo ni tofauti kwa kuwa kuna timu 16, hivyo hadi inafika
Sikukuu ya Krismasi, tayari mzunguko wa pili unakuwa umeanza.
Wakati
inafika Krismasi, tayari kila timu imecheza mechi mbili, maana yake
kila moja imefikisha mechi 17 na Simba ndiyo wako kileleni wakiwa na
pointi 41. Hapa unaweza kuona pia, ile maana ya kipimo cha Krismasi,
inaweza kutumika hata hapa nyumbani Tanzania kwa kuwa mara nyingi timu
inayokuwa juu hadi kipindi hicho, imetwaa ubingwa ingawa Tanzania
kumekuwa hakuna uhakika sana kama ilivyo Ulaya.
Timu
nyingi zilishindwa kubeba ubingwa licha ya kuwa kileleni mwa Ligi Kuu
Bara inapofikia mwisho wa Desemba kwa kuwa huenda ziliboronga katika
mechi zake tano za mwisho ambazo zinakuwa kati ya Aprili na Mei wakati
ligi inaisha.
Tanzania Bara:
Simba
ina pointi 41 ikiwa inafuatiwa na mpinzani wake namba moja Yanga ambaye
ana pointi 37 ikiwa ni pengo la pointi nne sasa baada ya Yanga
kulipunguza hadi kufikia pointi mbili tu badala ya nane.
Hadi
mechi ya 13, Simba ilikuwa kinara wa ligi, tofauti ya pointi zikiwa ni
nane, ikapoteza mechi ya 14 na 15, hivyo Yanga ikasogea na pointi kuwa
hizo mbili tu.
Baada
ya ushindi wa juzi, Simba imeongeza pengo hadi pointi nne kwa kuwa
Yanga ilipoteza hizo mbili baada ya sare ya 1-1 dhidi ya African Lyon
baada ya Amissi Tambwe kuisawazishia na bao hilo, halikusaidia kuipeleka
kileleni angalau kwa saa chache.
Nafasi
ya Simba kubeba ubingwa, huenda si sasa. Wanalazimika kushikilia hivyo
hadi watakapokutana na Yanga. Kama watawashinda, basi nafasi itakuwa
kubwa zaidi. Kwa mwendo wa ligi ya Tanzania Bara ambayo imejaa makosa ya
waamuzi, ujanja wa mipango ya nje uwanja. Si rahisi kusimama na kusema
Simba ina nafasi kubwa.
Premier League:
Chelsea
imeshikilia kileleni ikiwa na pointi 43, bado mechi mbili imalize
mzunguko wa kwanza. Liverpool inaonekana inaifutia kwa kasi kubwa, sasa
ina pointi 37.
Chelsea
ambao wameshinda mechi 11 zilizopita wako katika kasi nzuri lakini
watakaporejea, bado watakuwa na kazi ya kuamsha upya kasi ambayo kama
watafanikiwa kumaliza nayo vizuri mzunguko wa kwanza.
Kinachoonekana
Manchester City iliyo na pointi 36, bado ni mpinzani wa karibu lakini
utaona Arsenal ana 34, Tottenham na 33 na Manchester United amekusanya
30. Hautakiwi hata kidogo kuibeza hata moja kati ya hizo kwa kuwa safari
bado ni ndefu sana.
La Liga:
Huku
ni mbio za watu wawili, vigogo Real Madrid na FC Barcelona. Mara nyingi
akiongezeka atakuwa mmoja Atletico Madrid, Sevilla au Villarreal.
Madrid wako kileleni na pointi 37 lakini wana mchezo mmoja pungufu huku Barcelona wakiwafuatia na pointi 34.
Sevilla
wameamka kwenye La Liga safari hii, maana wanaipa Barcelona presha
kubwa kutokana na pointi 33 walizokusanya wakiwa na michezo 16 sawa na
wao.
Kwa
hali inavyokwenda na kiwango cha juu cha Madrid kama watamalizana nacho
mzunguko wa kwanza, maana yake watakuwa na kazi ya kukiinua mzunguko wa
pili. Wakiteleza, Barcelona, Sevilla hawako mbali.
Bundesliga:
Bayern
Munich ni kama wamejimilikisha kombe hilo kwa kipindi kirefu kidogo.
Sasa kuna ugumu kwa kuwa RB Leipzig iko nyuma kwa tofauti ya pointi tatu
tu.
Bayern
wana 36, Leipzig wana 33. Bayern walipata pointi tatu zaidi baada ya
kuifunga timu hiyo waliyokuwa wakilingana nayo pointi baada ya kila timu
kuwa imecheza mechi ya 15.
Hata
kama Bayern imekwenda Krismasi ikiwa kileleni, bado inaonyesha kazi ni
ngumu kwa kuwa wao wameshinda mechi zote 5 zilizopita na Leipzig
walikuwa wameshinda tano kabla ya wao kuwafunga.
Serie A:
Juventus
ambao hawajafungwa mechi tatu zilizopita ndiyo wamekuwa watawala wakuu
wa Serie A kwa miaka mitano. Krismasi yao wako kileleni na imekwenda
vizuri. Wao wana sifa ya kusimamia vizuri mwenendo wao baada ya kufika
kileleni. Wamefanya hivyo kwa miaka mitatu iliyopita.
AS
Roma ambao hawajafungwa mechi tisa zilizopita, wako katika nafasi ya
pili wakiwa na pointi 38, tofauti ya nne tu na Juventus. Rekodi
inaonyesha wamekuwa wakifanya hivyo na mechi tano za mwisho wanashindwa
kusimama imara na Juve wanachukua ndoo.
Ligue 1:
Nice ya Mario Balotelli ndiyo vinara, wana pointi 44 wakiwa wamemaliza mzunguko wa kwanza safi kabisa.
Vigogo
Monaco wana pointi 42 katika nafasi ya pili, PSG wana 39 katika nafasi
ya tatu. Hakuna ubishi vigogo hawa watakwenda kujipanga.
Nice
hawajafungwa mechi 7 zilizopita, Monaco hawajafungwa 4 zilizopita huku
PSG wakiwa hawajapoteza hata moja katika mechi 10. Hii inaonyesha
mzunguko wa pili, Nice wanalazimika kufunga mkanda hasa hata kama
walikula Krismasi, kileleni.
0 Maoni:
Post a Comment