JUSTICE ZULU AKIWA NA WAZIRI MWIGULU. |
Kiungo Justice Zulu maarufu kama "Mkata Umeme", anaweza kuanza kucheza katika mechi zinazofuatia za Yanga.
Suala la kutumika kwa Zulu litakuwa ni la Kocha George Lwandamina kwa kuwa sasa kila kitu safi.
Tayari
uongozi wa Yanga umelishughulikia suala la vibali vya mchezaji huyo,
hasa kile cha kufanya kazi nchini ambacho awali hakikuwa kimekamilika.
Lakini
mwenyewe anaonekana kuwa yuko fiti tayari kwa mechi kwa kuwa amekuwa
akiendelea kufanya mazoezi binafsi kuhakikisha anakuwa fiti zaidi.
Zulu amejiunga na Yanga akitokea Zesco ya Zambia, lakini kabla hakuwa amecheza mechi ya mashindano kwa zaidi ya miezi minne.
Kutokana na hali hiyo, ameonekana kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuhakikisha anafanikiwa kurejea katika kiwango chake.
Kabla,
Yanga ilimpanga katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa kwanza lakini
suala la kukosa kibali cha kazi, ilichangia aondolewe kwenye listi
katika dakika za mwisho kabisa.
0 Maoni:
Post a Comment