Katika mchezo pekee wa ijumaa usiku wa ligi kuu ya Uingereza iliyowakutanisha HULL CITY VS EVERTON ambapo Everton walisawazisha Dakika ya 84 kwa Bao la Ross Barkley na kupata Sare ya 2-2 walipocheza na Hull City huko Kingston Communications Stadium kwenye Mechi pekee ya EPL, Ligi Kuu England.
Matoke hayo yamewatoa Hull kutoka mkiani na sasa wapo Nafasi ya 19 huku Everton wakibakia Nafasi yao ile ile ya 7.
Hull walitangulia kufunga kwa Bao la Michael
Dawson na Everton kusawazisha Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza
baada ya Kipa David Marshall kupanchi Mpira wa Kona ya Kevin Mirallas na
kutumbukia wavuni.
Frikiki ya Robert Snodgrass iliwapa Hull uongozi wa 2-1 lakini Barkley akawapa Sare ya 2-2.
MAGOLI:
Hull City 2
Dawson 6'
Snodgrass 65'
Everton 2
Marshall 46', Amejifunga Mwenyewe
Barkley 84'
Leo
zipo Mechi 7 za EPL za kufunga Mwaka na mechi ya mwisho kabisa ni ule
Mtanange mkali huko Anfield kati ya Liverpool na Manchester City.
VIKOSI:
Hull City: Marshall; Maguire, Dawson, Davies; Elmohamady, Livermore, Meyler, Diomande, Robertson; Snodgrass, Mbokani.
Akiba: Jakupovic, Huddlestone, Clucas, Maloney, Weir, Henriksen, Mason.
Akiba: Jakupovic, Huddlestone, Clucas, Maloney, Weir, Henriksen, Mason.
Everton: Joel; Coleman, Jagielka, Williams, Baines; Gueye, Barry; Valencia, Barkley, Mirallas; Lukaku.
Akiba: Hewelt, Funes Mori, Holgate, Cleverley, Davies, Lennon, Calvert-Lewin.
Akiba: Hewelt, Funes Mori, Holgate, Cleverley, Davies, Lennon, Calvert-Lewin.
REFA: Jon Moss
0 Maoni:
Post a Comment