TAIFA JANG'OMBE YAWATUNGUA WAPINZANI WAO KATIKA MAPINDUZI CUP

Tokeo la picha la kombe la mapinduzi logo
MASHINDANO ya Kombe la Mapinduzi ya kuenzi Mapinduzi yanayofanyika katika Visiwa vya Zanzibar na Pemba yameanza Usiku wa kuamkia leo huko Amaan Stadium, Zanzibar. Timu ya Taifa Jang’ombe kuifunga Jang’ombe Boys 1-0 kati Mechi ya Kundi A.
Bao la ushindi la Taifa Jang’ombe lilifungwa Dakika ya 83.
Michuano hii imegawanyika katika Makundi Mawili. Kundi A lina timu za Simba ya Dar es Salaam, Taifa ya Jang’ombe, Jang’ombe Boys, KVZ na Mabingwa Watetezi, URA ya Uganda.
Kundi B lina Timu za Yanga, Azam FC, Jamhuri na Zimamoto.

MAKUNDI:

KUNDI A
-Simba
-Taifa Jang;ombe
-Jang’ombe Boys
-KVZ
-URA [Mabingwa Watetezi, Toka Uganda]

KUNDI B
-Yanga
-Azam FC
-Jamhuri
-Zimamoto

Baada ya Mechi hii ya disemba 30, Januari 1 Mabingwa Watetezi, URA watacheza na KVZ kuanzia Saa 10 Jioni na baadae Simba kumenyana na Taifa ya Jang'ombe Saa 2 na Nusu Usiku.

Mechi za Kundi B zitaanza Januari 2, kwa Azam FC kucheza na Zimamoto kuanzia Saa 10 Jioni na Yanga kuivaa Jamhuri Saa 2 na Nusu Usiku.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment