Muunganiko wao umekuwa wa faida ya moja kwa moja klabuni kwa kuzalisha magoli mengi ambayo yamekuwa ndiyo msaada ndani ya timu
Mzunguko wa pili Ligi Kuu Tanzania Bara ulianza wikendi iliyopita kwa
timu zote kushuka dimbani kusaka alama tatu muhimu, klabu za Simba na Yanga zimeendelea kuchuana kwa karibu kwenye mbio za ubingwa huku Azam, Kagera na Mtibwa wakikabana koo kwenye nafasi ya tatu na ya nne.
JKT Ruvu mambo siyo mazuri kwao kwani ndiyo wana kamata mkia kwenye
msimamo, Toto Africa, Majimaji na Mwadui hawapo mbali nao kwenye hati
hati ya kushuka daraja
Ukiachana na msimamo wa Ligi, msimu huu zimejitokeza kombinesheni
nyingi kwenye klabu ambazo zimezalisha magoli mengi katika michezo 16 tu
mpaka sasa na ambayo yamekuwa na faida ndani ya timu zao
KIUNGOMSHAMBULIAJI inakuletea kombinesheni bora na zilizo zalisha magoli mengi mpaka sasa nusu msimu
Ndiyo muunganiko ulio zalisha magoli mengi Ligi Kuu kuliko zote,
Msuva pekee amefunga magoli 9 na kutengeneza magoli kumi na tatu kwa
wenzake huku Niyonzima akifunga goli moja na kuchangia mengine zaidi ya 5
Wachezaji hawa wa zamani kutoka Mtibwa wamefanikiwa kutengeneza
ushirikiano mzuri ndani ya Msimbazi, katika michezo 16 ya Ligi Kuu
viungo hawa wamefunga magoli 15, Kichuya amefunga magoli 9 na Muzamiru 6
pia wakitengeneza mengine zaidi ya 7 kwa wengine.
lya Ndanda imefanikiwa kufunga magoli 15 katika michezo 16, katika
magoli 15 timu iliyo funga msimu huu asilimia 75 yamefungwa na
kombinesheni ya Mponda na Riffat Khamis, washambuliaji hawa kila mmoja
ametikisa nyavu mara tano.
Chachu ya Mtibwa kufanya vizuri msimu huu ni uwepo wa ushirikiano
mzuri kati ya Mandawa na Haruna Chanongo, wamekuwa na msaada mkubwa
klabuni, washambuliaji hawa kwa pamoja wamefunga magoli 13, Chanongo
magoli 6 huku Mandawa 7
0 Maoni:
Post a Comment