WAKATI
Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea, wakiwa na uhakika wa kumaliza
Mwaka huu 2016 wakiongoza Ligi, vita kubwa ipo huko Anfield hii Leo
ambako Liverpool wanapambana na Manchester City kuwania nani atafunga
Mwaka akiwa Nafasi ya Pili.
Chelsea wapo kileleni wakiwa na Pointi 46, Liverpool wanafuata wakiwa na Pointi 40 na City ni wa 3 wakiwa na Pointi 39.
Leo
Chelsea watacheza mapema kwao Stamford Bridge na Stoke City na kuacha
zigo kubwa kwa Liverpool na Man City kupigana baadae Usiku.
Kitu chema kwa City ni kurejea tena dimbani kwa Straika wao mkuu Sergio Aguero aliyekuwa Kifungoni kwa Mechi 4.
Lakini
Klabu zote zina Majeruhi kadhaa na kwa Liverpool hao ni Grujic,
Coutinho, Matip, Bogdan na Ings wakati wa City ni Kompany, Delph na
Gündogan.
Kwenye Mechi kama hii iliyochezwa Anfield Msimu uliopita Last season Liverpool 3 Manchester City 0.
Mameneja Wameongea nini kuhusu mechi hii?
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp: "Hii ni Gemu kubwa kwa kila Timu. Klabu 6 zinagombea Nafasi 4 au moja. Kila Gemu ni kama Fainali.”
“City wana vipaji kwenye Timu yao na Benchi lao. Kitu cha maana kwetu ni kuchezea Anfield. Ni lazima tutumie hilo!”
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola: "Wao ni Wagombea Ubingwa. Nishawahi kucheza dhidi ya Jurgen Klopp, tunajuana. Anfield itawapa matumaini makubwa!”
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
LIVERPOOL: Mignolet, Clyne, Lovren, Klavan, Milner, Lallana, Henderson, Wijnaldum, Mane, Origi, Firmino
Akiba: Karius, Manninger, Can, Sturridge, Moreno, Lucas, Stewart, Randall, Brannagan, Ejaria, Gomez, Woodburn, Alexander-Arnold
MAN CITY: Bravo, Sagna, Otamendi, Stones, Clichy, Fernandinho, Toure, Silva, Sterling, Aguero, De Bruyne
Akiba: Caballero, Gunn, Navas, Adarabioyo, Nolito, Garcia, Maffeo, Tasende, Kolarov, Fernando, Iheanacho, Zabaleta
CRAIG PAWSON |
REFA: Craig Pawson
0 Maoni:
Post a Comment