PALE Utani
unapozidi ni shida, kwani Yanga ilipanga kuondoka leo saa 1:00 asubuhi
kwenda Zanzibar, lakini imelazimika kufuta safari yake baada ya kubaini
wangepanda boti moja na Simba katika safari yao.
Timu
zote hizo zinakwenda Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi
ambayo imeanza jana Ijumaa usiku kwa kushirikisha timu za Zanzibar,
Tanzania Bara na Uganda.
Mchezo
ulikuwa hivi, Yanga ilikatiwa tiketi ya boti ya Kilimanjaro kwenda
Zanzibar leo saa 1:00 asubuhi, walipododosa wakabaini katika boti hiyo
pia kikosi cha Simba kitakuwemo.
Kuona
hivyo, viongozi wa Yanga wakalazimika kubadili tiketi za timu yao na
kusogeza muda hadi saa 9:00 alasiri watakapoanza safari lengo likiwa ni
kutopanda boti moja na Simba.
Mmoja
wa viongozi wa Yanga, alilithibitishia Championi Jumamosi kuhusu hali
hiyo na kusema sasa kila kitu kipo sawa na wao watapanda boti yao
alasiri na siyo ile ya asubuhi na Simba.
“Hivi
itawezekana vipi mtu usafiri na adui wako? Kwetu hakuna kitu kama hicho
wao kama Simba wanaona sawa kusafiri na sisi kwenye boti sawa, lakini
sisi kwetu hapana hatuwezi,” alisema bosi huyo.
Alipotafutwa
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh kuzungumzia sakata hilo alisema: “Ni
kweli tulipanga tuondoke kesho (leo) saa moja asubuhi na boti la
Kilimanjaro, lakini tumebadili muda na tutaondoka saa tisa alasiri.”
Kwa
upande wa Simba, Mussa Mgosi alisema: “Sisi tunaondoka kesho (leo)
asubuhi na tutaondoka na kikosi chote tulichokisajili na nisingependa
kuwazungumzia wapinzani wetu."
SOURCE: CHAMPIONI
SOURCE: CHAMPIONI
0 Maoni:
Post a Comment